Na Mohab Dominick
Kahama,
Juni 24,2014
Muuguzi mmoja Juma Deo (29) wa Zahanati ya Bakwata Wilayani
Kahama mkoani Shinyanga ambaye ni mkazi wa Maswa Mkoani Simiyu, amenusurika
kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutelekeza mke na watoto wawili kwa madai
ya kutompenda mke wake.
Sakata hilo limetokea mwishoni wa juma lililopita katika Ofisi ya
Maendeleo ya Jamii ya Halmashauri ya Mji wa Kahama kufuatia malalamiko
yaliyofunguliwa na Veronika John(21) mke wa Deo mwenye watoto wawili mmoja wa
miaka minne na mwingine mwaka mmoja.
Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Regina
Nkwabi alisema kuwa Ofisi yake ilipokea
malalamiko kutoka kwa Veronika kabla ya kumwita Deo na kuwatambua watoto wake
aliowatelekeza pamoja na Mama yao.
Nkwabi alisema Ofisi yake ilipewa uwezo wa kumshauri mume
anapotelekeza watoto aweze kuwahudumia, na kwamba akikataa hufikishwa
mahakamani ambapo faini yake ni shilingi 5,000,000 au kwenda jela miezi sita; au
vyote kwa pamoja.
Veronika alikaa kwa wazazi wa Deo huko Maswa wakati wote Deo
alipokuwa akisoma katika Chuo cha uuguzi (PHN) cha mjini Kahama, na
alipoajiriwa hakurudi tena kwa mkewe hadi wazazi wa deo walipomfukuza Regina na
watoto wake.
Alipotakiwa kueleza sababu ya kutohudumia watoto wake, Deo alisema
alishindwa kutuma pesa kwa kuhofia Veronica angetumia vibaya fedha hizo huku
akiwa nauamuzi wa kuachana naye kwa kuwa ni mbishi, na kwamba tayari alipata
mchumba mwingine wilayani Kahama.
Kufuatia maelezo hayo Ofisi ya Usatawi wa Jamii ilimwamuru
Deo kuweka mkataba wa kumpangishia nyumba ya kuishi Veronika na watoto wake,
kutoa mahitaji ya kila siku na kumwanzishia Regina mradi ili aweze kujitegemea
kiuchumi.
Tukio hilo lilitokea siku chache tu tangu Kauli ya Mkuu wa Wilaya
ya Kahama Benson Mpesya kuwaagiza watendaji wa Kata kuwashughulikia wanaume
wanaolalamikiwa na wanawake waliozaa nao kutelekeza watoto wakilelewa na mama
zao peke yao. mwisho
No comments: