Na Mohab Dominick
Shinyanga
July 25,2014
Kikongwe sayi (75)mkazi wa kijiji cha mwagata kata ya
mwamalili manispa ya shinyanga ameuwa
kikatili kwa kukatwa na mapanga
sehemu mbalimbali za mwili wake na kufariki dunia.
Kamanda wa polis mkoa wa shinyanga justu kamugisha
amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo limetokea majira
ya saa tano za usiku kwa kikongwe huyo .
Akifafanua zaidi kamanda alisema kuwa wakati kikongwe huyo amelala na wajukuu wake wawili ghafla alivamiwa
na watu wawila ambao akuwafahamu na
kumcharanga na mapanga.
.
Aidha kamanda alisema
kuwa walimcharanga sehemu mbali mbali za mwili wake ikiwemo shingo ,mabenga
,ali ambayo ilipelekea mauti yake kikongwe huyo .joel machia (45)mkazi wa
mwamalili anashikiliwa kwa tuhuma hizo
na kwamba uchunguzi wa jambo hili unaendelea .
Kamanda justu pia
amesema kuwa jeshi la polisi katika
uchunguzi wa awali limebaini kuwa chazo cha ugomvi huo ni kugombea mashamba .
Aidha mkoa wa shinyanga umekuwa na matukio ya mara kwa mara
ya ukatili wa vikongwe katika mkoa huo jambo ambalo linatia shaka maisha yao
kwa mwezi huu ni kikongwe wa 4 tiali
wamekwisha uawa kwa dhima hiyo ya mashamba na uchawi.
mwisho
No comments: