karibu naibu waziri Godfrey zambi katika kiwanda chetu cha kom oil mill ltd.
wafanyakazi wa kiwanda cha kom oil mill ltd wakimpokea naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika katika kiwanda hicho mbele ni mbuge wa jimbo la kahama jemes lembeli .
naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika Godfrey zambi akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni katika ofisi ya mkurungezi wa kom oil mil ltd kulia alisimama ni mkurungezi mkuu wa kom oil mill mhoja ndegesela.
naibu waziri wa kilimo na chakula na ushirika akisisitiza jambo mbele ya mkurungezi wa kom oil mill ltd kabla kuanza kukangua kiwanda hicho mwenye kofia nyeupe ni mkurungezi wa kom oil mill ltd mhoja ndengesela..
naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika Godfrey zambi mwenye miwani akiwa na na mwenyeji wake mkurungezi wa kom oil mill ltd mhoja ndengesela kukangua kiwanda hicho.
naibu waziri mwenye suti yakijivu wakitembelea kiwanda cha kom oil ltd .
moja ya bidha zinazodhalishwa ndoo za plastiki kiwanda cha kom oil mill ltd .
wafanyakazi wa kiwanda cha kom oil mill wakisukuma pamba kuingia kwenye bomba la kupeleka pamba kwenye mashine.
naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika akikangua kiwanda cha kom oil mill ltd .
mwenye kofia nyeupe ni mkurungezi mtendaji wa kampuni ya kom oil mill ltd mhoja ndegesela akimuonyesha naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika mabati ya aina mgongo maarufu kwa jina la msumbiji ambayo tanatengenezwa katika kiwanda hapa .
baadhi ya wafanyakazi wa kom oil mill ltd .
mwenye kofia nyeupe na shati nyeupe ni mkurungezi wa kom oil mill ltd mhoja ndengesela akitoa maelezo kwa naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika Godfrey zambi juu ya udhalishaji wa mabati katika kiwanda hicho na kero ya umeme inayojitokeza mara kwa mara na kupungunza udhalishaji wa mabati hayo.
wanyafakazi wakionyesha jinsi gani bati linavyotengenezwa kwa naibu waziri ambapo alitembelea kiwandani hapo .
baadhi ya wafanyakazi wa kom oil mill ltd.
naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika Godfrey zambi akiwa na mkurungezi wa kom oil mill ltd mhoja ndengesela ndani ya kiwanda cha kuchambua pamba.akimpa maelekezo juu ya udhalishaji unaokwamishwa na umeme kuwa ndogo na kiwanda kufanya kazi chini ya miezi mitata badala ya mwaka au miezi minane .
wafanyakazi wakiweka rola la bati kwenye mashine ya kutengeneza mabati wakimuonyesha naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika.
naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika Godfrey zambi karibu sana kiwandani kwetu hayo ni maneno anasema mkurungezi wa kom oil mill ltd mhoja ndengesela kwa mgeni wake .
baadhi ya wafanyakazi wa kom oil mill ltd wakisikiliza hotuba ya naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika.hayupo picha .
mcheleshaji wa kiwanda cha kom oil mill ltd victor tandise akimkribisha mgeni naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika Godfrey zambi hayupo picha kwenye eneo la mkutano na wafanyakazi wa kom oil mill ltd.
baadhi ya wafanyakazi wakisikila kwa makini hotuba ya naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika Godfrey zambi.
mkurungezi wa kampuni ya kom oil mill ltd mhoja ndengesela wakati wa mkukaribisha naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika kwenye mkutano na wafanyakazi wa kampuni hiyo .
picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya kahama na kampuni ya kom oil mill ltd .
mh hii ndiyo mali za hapa nchini kwetu hayo ni maneno anasema mkurungezi wa kampuni ya kom oil mill ltd mwenye kofia nyeupe mhoja ndengesela kwa naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika Godfrey zambi mwenye miwani
viwanda vyetu hivi waziri .
naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika Godfrey zambi akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya kom oil mill ltd .
naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika akisisitiza jambo kwa mkurungezi wa kom oil mill ltd mwenye kofia nyeupe jambo jema la kuhekeza hapa nyumba na kikubwa ni hapa nchini kwako .
naibu waziri akisoma hotuba nmbele ya wafanyakazi wa kom oil mill ltd .
mali yetu waziri hii inatoka hapa kahama .hayo ni maneno ya mkurungezi wa kom oil mill ltd mhoja ndengesela kwa naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika.
naibu waziri akiangalia uchambuzi wa pamba katika mashine mpya za kisasa mwenye suti ya kijivu ni waziri Godfrey zambi .
naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika Godfrey zambi mwenye miwani akiangalia jiko la pumba la kuchemshia mafuta pindi umeme hakuna mwenye kofia nyeupe ni mkurungezi wa kom oil mill ltd mhoja ndengesela.
Na Mohab
Dominick
Kahama
Julay 2, 2014.
SERIKALI
imepiga Marufuku utozwaji wa Ushuru wa asilimia tano wa fedha za zao la
Pamba kutoka kwa Wanunuzi wa zao la hilo kwa Halmashauri 21 hapa nchini
zinazolima zao hilo na badala yake Serikali ndio itawajibika kulipa asilimia
hiyo.
Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Godfrey
Zambi aliyasema hayo wakati akikagua kiwanda cha kuchambulia Pamba cha Kahama
Oil Mills huku akikazia kauli ya Waziri Mkuu Mizengo aliyoisema hivi karibuni
na kuongeza Serikali ndio itakayowajibika kuilipa Halmashauri husika kiasi
hicho cha fedha.
Zambi alisema kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika
kikao chao hicho cha Wadau wa Pamba walipendekeza zao hilo liuzwe kwa shilingi
750 wakati Serikali ilipendekeza liuzwe kwa shilingi 720 na kubeba mzigo huo wa
shilingi 30 kwa uilipa Halmashauri husika.
Naibu Waziri huyo alisema kuwa kwa kipindi cha Mwaka
huu 2014 jumla ya kilo milioni 235 za Pamba zinatemea kuvunwa katika kipindi
hiki ambazo ni kiwango cha Wastani kuliko miaka mingine ya nyuma na kuongeza
kuwa hali hiyo inatokana na hali ya hewa.
Awali katika Taarifa ilioyosomwa na Mkurugenzi wa
Kiwanda cha Kahama oil mill kwa niaba ya Makampuni ya ununuzi wa zao hilo
Mkoani Shinyanga Muhoja Nkwabi alisema wao kama wadau wakubwa wa zao walikataa
kulipoa ushuru wa asilimia tano kwa Halmashauri husika kutokana na baadhi ya
makampuni mengine kuzuiwa kununua zao la pamba Mkoani Geita kwa sababu ya
kutolipa ushuru huo.
Mhoja alisema kuwa Mkoani Geita kuna Kampuni moja
tuu ya ICK ambayo imepewa kibali na Bodi ya Pamba na Kamati za mazao ya Wilaya za Nyangwale na Sengerema huku
baadhi ya Makampuni mengine ya ununuzi wa Pamba kama Vile NIDA, KCCL na Kampuni
ya Fresho Investment yakinyimwa kununua zao hilo.
Alisema kuwa wao kama Makampuni yanaomba Wizara ya
Kilimo chakula na Ushirika kuwarudishia Mapuni hayo fedha zao ambazo ni kiasi
cha shilingi milioni 207.2 walizotoa kama utangulizi wa ushuru wa Pamba katika
Halmashauri mbalimbali zinazolima zao hilo
kama kigezo cha kupata kibali cha kununulia zao hilo katika Halmashiuri
husika
Mhoja alisema kuwa katika msimu wa 2014 dhima ya
utekelezaji wa kilimo cha mkataba na kufikia lengo kulinganisha Wilaya nyingine
ambazo hazikufanya ubaguzi Kampuni zilizomba kupitia Wizara ya Chakula kilimo
na ushirika kuweka makampuni mengi katika ununuzi wa Pamba na sio kama
ilivyowekwa Kampuni moja ya ICK katika Wilaya za Geita na Nyangwale.
mwisho
No comments: