naibu waziri Godfrey zambi mwenye miwani kushoto akisoma tarifa ya wilaya ya kahama juu ya zao la tumbaku kulia ni mkurungezi wa halmashauri ya ushetu isabela chilumba mwisho kuli mwenye shati nyeupe ni mbunge wa jimbo la kahama jemes lembeli .
mbunge wa kahama jemes lembeli akimkaribisha mgeni rasmi naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha ushetu .
mkurungezi wa halmashauri ya ushetu isabela chilumba akiongea na wanachi juu ya malipo ya wakulima wa zao la tumbaku katika kijiji cha ushetu wilayani kahama mkoani shinyanga .
mkuu wa wilaya ya ya kahama Benson mpesya akiwahutubia wanachi wa kata ya ushetu wilayani kahama mkoani shinyanga .
wanachi wa kata ya ushetu wakisikiliza hotuba ya naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika katika kijiji cha ushetu wilayani kahama .
mh mbunge jemes lembele akiwahutumbia wanachi wa kata ya ushetu mbele ya naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika wakati wa ziara yake ya siku mbili kwa wakulima wa zao la tumbaku wilayani hapa .
kikundi cha ngoma cha kinamama ambao wamezaa machapa uchenza ngoma hii ya kimila katika ziara ya naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika wilayani kahama
mkuu wa wilaya ya kahama Benson mpesya akiongea na wanachi wa kijiji cha ushetu wilayani kahama juu ya zao la tumbaku kabla ya mgeni rasmi naibu waziri wa kulimo chakula na ushirika Godfrey zambi wakati wa ziara yake ya siku mbili wilayani hapa .
mh mbuge wa jimbo la kahama jemes lembeli akitoa ufafanuzi kwa wanachi wa kata ya ushetuwilayani kahama juu ya wakulima wa zao la pamba ambao wanafanyiwa vitendo vya ubadilifu kwenye mazao yao mbele ya naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika wilayani kahama .
kaimu meneja wa mkimkoa wa zao la tumbaku albert charle akifafanua jambo kwenye mkutano wa hadhara ushetu .
kaimu meneja wa kimkoa wa kitumbaku wilayani kahama Albert charle akitoa ufafanuzi juu ya malipo ya tumbaku kwa naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika Godfrey zambi kwenye mkutano wa hadhara kata ya ushetu wilayani kahama .
Naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika Godfrey zambi akiongea na wanachi wa kijiji cha ushetu juu ya zao la tumbaku mkoani shinyanga wilaya kahama katika halmashauri ya ushetu.
Na Mohab Dominick
Kahama
July 2, 2014.
SERIKALI imesema kuwa ipo mbioni kumleta Mkaguzi
Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) kuja Wilayani Kahama kukagua katika vyama vya
Ushirika vilivyopo Wilayani hapa kufuatia Madai mengi ya ubadhilifu wa fedha
yakiwemo kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Kahama James Lembeli.
Hayo yalisemwa juzi na Naibu Waziri wa Kilimo
Chakula na Ushirika Godfrey Zambi wakati akiwahutubia Wananchi wa Kata za
Ushetu na Bulungwa katika Halmashauri ya Ushetu na kujibu baadhi ya kero
zilizotolewa na Wakulima mbalimnbali wa zao la tumbaku na Pamba ikiwemo kero
hiyo ya kukaguliwa kwa vyama vya ushirika.
Naibu Waziri huyo alisema kuwa Serikali imeamua
kumwita Mkaguzi huyo wa Hesabu za Serikali kuja kuangalia kama kutakuwa na
ubadhilifu wa fedha za Wakulima wa zao la Tumbaku kama ilivyobaini upotevu wa
Shilingi bilioni 12 huko katika Mkoa wa Tabora hivi karibuni.
Alisema kuwa Serikali haiwezi kuvumilia kama
kutakuwa na upotevu wa fedha za Wakulima na kuongeza kuwa katika ukaguzi
utakaofanyika pindi kukionekana kuwa kuna ubadhilifu wowote wa fedha za
Wakulima Serikali haitasita kuchukua hatua kali kwa wale wote waliohusika
katika upotevu huo wa fedha.
“Nilipata malalamiko mengi kuhusu kukaguliwa kwa
vyama vya ushirika hasa kutoka kwa Mbunge wenu James Lembel na Mbunge ndio kioo
cha Wananchi na sisi kama Serikali hatuwezi kupuuza malalamiko hayo na
tutayafanyia kazi haraka iwezekanavyo”, Alisema Godfrey Zambi Naibu Waziri wa
Kilimo chakula na Ushirika.
Awali akisoma Taafia ya Wilaya ya Kahama mbele ya
Naibu Waziri huyo, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya alisema kuwa baadhi
ya sababu zinazosababisha vyama vya msingi kushindwa kuendelea ni pamoja na
Wakulima kutorosha Tumbaku wanayovuna ili kukwepa madeni wanayodaiwa na vyama
vya msingi husika.
Mpesya alisema kuwa baadhi ya Wakulima wamekuwa
hawauzi Tumbaku katika vyama vya msingi walivyokopeshwa Pembejeo na kwenda
kuuza kwa magendo katika vyama ambavyo haviwajibiki na Mkulima huyo.
Pia alisema kuwa Changamoto nyingine ni pamoja na
Viongozi wa vyama vya Ushirika ushirika kuwa wabadhilifu wakubwa pamoja na
kutokuwa na Elimu ya kutosha ya kuwaongoza wakulima wao katika maeneo yao na
kuongeza kuwa alishawahi kuwaweka ndani viongozi 10 kutokana na ubadhilifu wa
fedha za wakulima.
mwisho
No comments: