Hili ndiyo eneo la mgodi wa vasista mines katika kijiji cha isonda wilayani nyanghwale mkoani Geita .
Mwenye kipasa sauti ni meneja mradi wa kampuni ya vasista Goodluk kafutila na mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya nyanghwale Ibrahimu marwa wakati wa kuweka jiwe la msingi katika mgodi huu .
Mkuu wa wilaya ya nyanghwale ibrahumu marwa ambaye anapinga makofi karibu sana katika mgodi wetu wa vasista mines .
Mkurungezi wa vasista mines Bhavan Rajesh akitoa neno kwa mkuu wa wilaya ya nyangwale njisi mgodi huu hutakapotoa huduma kwa mwanachi wa kijiji cha isonda wilaya hapa .
Meneja mradi Goodluck kafutila mwenye shart nyeusi akisalimiana na mkuu wa wilaya ya nyanghwale mwenye shati nyeupe ni mkurungezi Bhavan Rajesh wakati mkuu huyo wa kuweke jiwe la msingi
Mkurungezi wa mgodi wa visista mines Bhavan Rajesh wakati akitoa hotuba kwa mgeni rasmi
Wangeni walikwa wa kijiji cha isonda kata ya nyungwa wilayani nyanghwale .
Baadhi ya wakurungezi wa mgodi wa vasista wakiwa wanangalia usalama eneo hilo
Askari wa ulinzi wakiwa katika mkakati wa ulinzi wa kampuni visista mgodi huo .
Wafanyakazi wa mgodi wa visista wakiwa katika shughuli zao za madharizi ya mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya nyanghwale.
Mkuu wa wilaya ya nyanghwale Ibrahimu marwa akipewa maelenzo na meneja mradi goodluck kafutila
Mkuu wa wilaya ya nyanghwale akiwa katika picha ya pamoja na wana kijiji cha isonda wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi wa mgodi huu .
Mwenye sharti ya rangi ya maziwa kati wa nne mkuu wa wilaya ya nyanghwale Ibrahimu marwa akiwa picha ya pamoja na uongozi wa mgodi wa vasista mines mwenye sharti nyeusi ni meneja mradi goodluck kafutila .
Mwenye kuonyesha mkono ni meneja mradi wa mgodi wa vasista mines maeneo ya mgodi huu
Baadhi ya majengo ya ofisi za vasista mines katika kijiji cha isonda
Pia mapochopocho yalikuwepo bana wewe wacha tu hii ni habari nyingine
Huu ni mtambo mdogo wa uchenjuaji wa dhahabu wa bila kutumia madawa .
Wafanyakazi poa tu
Burundani kwa wazee wa kijiji cha isonda baada ya kuweka jiwe la msingi na mkuu wa wilaya ya nyanghwale Ibrahimu marwa .
Baadhi ya wakurungezi na watumishi wa vasista mines wakijadiliana juu ya mambo yalivyokwenda wakati wa uzinduzi huu.
Pia utunzaji wa mazingira upo kama jinsi vitalu vya miche vikiwa vimeoteshwa
Mkurungezi wa mradi katika mgodi wa vasista mines Goodluck kafutila akitoa neno la shukurani kwa mgeni rasmi .
Mkuu wa wilaya ya nyanghwale Ibrahimu marwa akiutubia wanachi wa kijiji cha isonda hawapo pichani wakati wa kuweka jiwe la msingi mgodi hapa .
Na
Mohab Dominick
Nyang’hwale
Agust
7 , 2014.
WANANCHI
wa Kijiji cha Isonda Kata ya Nyugwa Wilayani Nyang’wale Mkoani Geita wametakiwa
kujenga mahusiano mazuri na Wawekezaji waliopo katika Kijiji hicho kwa lengo la
kufaidika na huduma mbalimbalimbali za kijamii ili kuharakisha maendeleo
yao.
Diwani
wa Kata hiyo Donard Kaboroso aliyasema hayo juzi wakati wa uwekaji wa jiwe za
msingi wa Mwekezaji kutoka India kampuni ya Vasista itakayo juhusisha na
uchenjua wa Madini ya Dhahabu katika katika kijiji cha Isonda.
Kaboroso
alisema kuwa Wananchi wa Isonda wakiwa na mahusiano mazuri na Mwekezaji huyo
wanaweza kupata faida nyingi hasa katika mambo mbalimbali ya Kijamii kama vile
Elimu Afya hali ambayo itaweza kuleta mabaliko makubwa katika Kijiji hicho na
Wilaya ya Nyang’wale kwa ujumla.
Nae
Meneja Mradi wa Mradi wa Kampuni ya Vasista Goodluck Kafutila akisoma Taarifa
ya ujenzi wa Mgodi huo mbele ya Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya
ya Nyang’wale Ibrahimu Marwa alisema kuwa Kampuni ya Vasista imeingia ubia na
waafrika na kuongeza kuwa Mgodi huo pia utafanya kazi bila ya kutumia Kemikali.
Kafutila
alisema kuwa Mgodi huo ambao unategemea kukamilika ujenzi wake mwezi desemba mwaka
huu utatoa ajira kwa wataalamu mbalimbali wa madini wazawa na kuongeza kuwa
jumla wafanyakazi zaidi ya 100 watapata ajira kupitia mgodi huo ikiwa ni pamoja
na wakazi wa Vijiji vya jirani.
Pia
alisema kuwa mbali na ajira pia Mgodi huo pia utasaidia katika Wanakijiji wa
Isonda katika sekta za Kilimo cha umwagiliaji maji, umeme wa mionzi ya jua
pamoja na kutoa Elimu ya utunzaji wa mazingira kwa watu wa Kijiji hicho hali
ambayo italeta mabadiliko kuliko ilivyokuwa hapo awali.
Alisema
kuwa faida nyingine watakayaopata wanakijiji wa Kijiji hicho ni pamoja na
kupata fura kubwa ya kuuza bidhaa zao katika Mgodi huo kama vile mbogamboga
ambazo zitakazokuwa zikilimwa katika eneo hilo hali ambayo itakuza kipato cha
mtu mmoja mmoja katika eneo hilo na kuleta mabadiliko.
Aidha
Kafutila alisema kuwa Mgodi huo wa Vasista utakuwa na uwezo wa kusindika tani
10 za udongo kwa saa ikiwa ni sawa na tani 140 za udongo kwa siku kiasi ambacho
ni kikubwa kulinganisha na uwezo wa uzalishaji wa Mgodi huo.
Kwa
upande wake Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale
Ibrahimu Marwa alisema kuwa kazi kubwa ya Serikali ni pamoja na kuhakikisha
inaweka mazingira mazuri kwa wawekezaji hapa nchini ili watanzania waweze
kunufaika na rasilimali zao zinazowanguka katika maeneo yao.
Mwisho.
No comments: