Askari Polisi wakiwa eneo la tukio ikiwa ni kuimarisha ulinzi.(Picha Zote na demasho.com)
Eneo la tukio ambalo kitu kinachosadikiwa likiwa limezungushiwa alama na Jeshi la Polisi.
Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwangu akizungumza jambo na waandishi wa habari
katika hoptal ya mkoa wa Ruvuma baada ya kuwatembelea majeruhi hao.
Kamati ya ulinzi na Usalama wakiwa Hospital ya mkoa wa Ruvuma.
Aliyelala kitandani ni WP ambaye amejeruhiwa akiwa amelazwa katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma.
Askari Ramadhani Ally akiwa anaelezea jinsi mkasa huo ulivowakuta wakiwa kazini.
Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr Daniel Malekela akizungumza na wandishi wa habari hopitalini hapo.
Na Mohab Dominick
ASKARI watatu
wa jeshi la Polisi wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma
(Homso) iliyopo mjini songea Mkoani humo wakiwa wanapatiwa matibabu ya
majeraha ambayo waliyapata baada ya kushambuliwa kwa kitu kinachodhaniwa kuwa
ni Bomu la kurushwa kwa mkono.
Tukio hilo
limetokea September 16, 2014 majira ya saa moja na nusu usiku katika kata
ya Msufini karibu na daraja la Matarawe, wilayani Songea Mkoani Ruvuma
ambapo watu watatu wasio fahamika walitupa kitu kinacho sadikiwa kuwa ni Bomu
la kutupwa kwa mkono ambalo limetengenezwa kienyeji na kuwajeruhi askari
hao watatu waliokuwa doria.
Askari hao
waliojeruhiwa ni WP. 10399 PC Felista aliyejeruhiwa mguu wa kulia
kwenye unyayo na pajani ,G. 7351 PC Ramadhani aliye jeruhiwa mguu wa
kulia karibu na goti na tumboni upande wa kulia na G. 5515 pc John
aliyepata majeraha katika mguu wa kulia chini ya goti na jeraha dogo tumboni.
Mganga mkuu wa
Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr. Daniel Malekela ameeleza kutoa vipande vya bati
na misumari katika majeraha ya askari hao na mpaka sasa wanaendelea na
matibabu.
Alisema kufutia hali
hiyo Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linaendelea na uchunguzi wa kina ili
kuwakamata wahusika wa tukio hilo kwa hatua zaidi za kisheria.
Kwa upande wake Mkuu
wa mkoa wa Ruvuma Said mwambungu, amesikitishwa na kitendo hicho cha wahalifu
kujeruhi askari tena kwa makusdi na amesema serikali kupitia vyombo vyake vya
ulinzi na usalama watahakikisha wanawasaka na kuwakamata.
Mwisho
No comments: