Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mafunzo ya men engage meneja wa mradi huu emma mashobe mwenye miwani .
waandishi wa habari wakimskiliza meneja wa mradi wa men engage kwenye mafunzo ya vitendo yanafanyika mjini kahama mafunzo haya ni siku tatu .
waandishi wa habari wa radio kaham fm mwenye shati ya blue bakari haridi na mwenye gauni la kitenge ni mwaandishi wa faraja fm gema wakisikiliza kwa makini emma mashobe wakati wa maswali na majibu juu ya usawa wa kijinsia .
Mwaandishi wa ITV steven wanganyi akitoa maelezo juu ya mafunzo ya men engage .
Meneja wa mradi wa men engage emma mashobe akitoa somo la kuhamashisha wanaume na wavulana katika kuleta usawa wa kijisia kwa waandishi wa habari .
Emma mashobe akionyesha jinsi hali hilivyo katika usawa wa kijinsia katika mafunzo ya vitendo kwa waanahabari .
Mwenye miwani meneja wa mradi wa men engage Emma mashobe wakati wa majadiliano kwa waadishi wa habari.
Imeelezwa, mabadiliko ya kutoka
maisha ya kuwabagua wanawake kuelekea usawa wa kijinsia ni jukumu la jamii nzima na wala siyo la
wanawake wenyewe na wanaharakati wa masuala ya jinsia peke yao.
Hayo yamebainishwa mjini Kahama, kwenye semina ya waandishi wa
habari wa shinyanga, semina iliyoandaliwa na shirika la care international
Tanzania , linalotekeleza Mradi wa ushirikishwaji wa wavulana na wanaume katika
kuleta usawa wa kijinsia (men engage).
Akifungua Semina hiyo ya siku tatu,
meneja wa mradi huo Emma Mashobe amesema, kwa kipindi cha miaka miwili umeweza
kuleta mabadiliko makubwa kwani jamii imeanza kuelewa umuhimu wa haki na usawa
wa kijinsia.
Mashobe amesema, mradi umekuwa
ukiwaelimisha wavulana mashuleni kupinga dhuluma kwa wasichana na kuhamasisha
jamii kutambua mchango wao kwa familia na jamii kwa ujumla, na kwamba wanapaswa
kupata stahiki zote ndani ya jamii.
Afisa ubora na mafunzo wa mradi
David Magige amesema, kushirikishwa kwa wanaume na wavulana katika mradi
kunatokana na ukweli kwamba mila na desturi za eneo hilo bado zinatambua mtoto
wa kike kama chanzo cha uchumi kwa familia.
Amesisitiza, mabadiliko ya kweli
yatawezekana tu iwapo wavulana na wanaume wataacha kuwaona wasichana kama
sehemu ya burudani huku wakiwapa mimba na kuwaachisha masomo chanzo cha kuwepo
kwa umaskini na ufukara kwa jamii.
Mradi wa Men Engage unatekelezwa kwa
miaka mitatu wilayani Kahama huku ukihusisha kata za Bulyanhulu, Bugharama na
Lunguya zilizoko katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama.
Semina hiyo imehusisha waandishi wa
habari 15 kutoka vyombo vya habari mbalimbali mkoani Shinyanga, kwa kuwa ndiyo
vyombo vinavyoweza kufikisha haraka ujumbe kwa watu wengi na kwa mara moja.
MWISHO
No comments: