Hapa ni majadiliano hawa askari jamaa wako wape hayo ni maneno ya polisi kuhangalia hali ya usalama jijini
Mwandishi wa habari Badi
akilia baada ya kushambuliwa na Polisi,huyu ni moja ya waandishi
walioshambuliwa
Ili kuzibidhibiti hali ya ulinzi jiji dar polisi waliweka ulinzi mkali sana kila eneo la jijini kama polisi wanavyoneka na mbwa zao barabarani
TWende huku tulia hii ndiyo hali ilivyokuwa katika jiji la dar
Wewe tulia hapo hupo chini ya ulinzi
Hivi ndiyo hali hilivyokuwa jiji ulinzi mkali kuliko maelezo .
Kuna taarifa kuwa
mwaandishi wa habari wa IPP Media kapigwa na jeshi la polisi alipokuwa ameenda
kuripoti matukio yaliyokuwa yanaendelea baada ya mwenyekiti wa CHADEMA Mhe,
Mbowe alipoenda kuitikia wito wa jeshi hilo la polisi.
Habari zinasema kuwa
baada ya Mbowe na wanasheria kuingia ndani polisi walianza kupiga kila
aliyekuwa eneo la tukio bila kujali ni nani ndipo alipojikuta mwandishi huyo
akipigwa mpaka kupoteza fahamu.
Imeelezwa
kuwa waandishi wengi wa habari wameumia vibaya kutokana na kukimbizwa na mbwa
wa polisi huku wengine wakiumwa na mbwa hao.
Waandishi
wa habari wameshindwa kutimiza wajibu wao kwa kuzuiwa na polisi ambao
wameshindwa kutambua uwepo wa waandishi wa habari,Je Uhuru wa vyombo vya habari
uko wapi Tanzania? na kama waandishi wa habari wameanza kuumizwa mapemaa kabisa
kabla hata kampeni za uchaguzi hazijaanza,Sijui uchaguzi ukifika hali itakuwaje!!
Ikumbukwe kuwa Mwaka
jana mwandishi wa habari Daud Mwangosi aliuawa kikatili kwa amri ya RPC
(Kamuhanda) wa Iringa wa wakati huo ambaye baada ya kutimiza azima yake hiyo
alipandishwa cheo.
Mami ya watu leo wamejitokeza kumsindikiza Mwenyekiti wa Taifa
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, baada ya
kuhitajiwa kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini, jijini Dar es
Salaam kuhusiana na kauli yake aliyotoa Septemba 14 mwaka huu,juu ya kuitisha
maandamano nchi nzima kupinga kuendelea kwa Bunge Maalum la Katiba.
Kilichofuata ni polisi kuamuru watu wote waondoke eneo hilo kwa
umbali wa mita 200 ambapo walikimbizwa na mbwa wa polisi na kusababisha wengi
wao waumie na kupoteza vitu vyao mbalimbali, hususani wanahabari ambao baadhi
yao waliumia na kupoteza zana zao za kazi
No comments: