Mkurungezi wa halmashauri ya mji wa kahama Felix kimario akitoa pongezi kwa uongozi wa mgondi wa buzwagi kwa msaada wa vitanda 27 katika hospital hiyo.vitanda hiyo vyenye samani ya milioni 54 .
Mkuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesya akiongea na wanganga na waunguzi wa hospila ya wilaya ya kahama kwenye makabidhiano ya vitanda 27 katika hosptali ya halmashauri ya mji mwenye kofia ni meneja undelezaji wa mgodi wa buzwagi George mkanza wakatika wa mabidhiano katika viwanja vya hosptali hiyo .
Katika
makabidhiano hayo Mpesya amesema ameshangazwa na mgawanyo wa kiutawala wa
wilaya ya Kahama iliyogawanywa kwenye halmashauri tatu za Mji,Ushetu na Msalala
mgawo huo umeathiri huduma za afya.
Aidha Mpesya
amesema mgawo huo pia umekwenda sambamba na hospitali ya wilaya ambayo nayo
imegawanywa katika Halmashauri tatu hali iliyodhoofisha utendaji kazi kwa
kuwagawa madaktari katika halmashauri tatu,badala ya kuimarisha moja ya wilaya.
Alipendekeza
Madiwani hao wangeweza kutumia busara wakaacha kuigawa hospitali hiyo ambayo
imesimama kama ya Rufaa kwa kutoa huduma kwa wagonjwa wanaotoka katika
Halmashauri zao,badala ya kuwapeleka Madaktari kwenye zahanati za vijiji,huku
wilaya kukiwa na mapungufu.
Naye
Meneja Uendelevu wa Mgodi wa Buzwagi George Mkanza amesema vitanda hivyo
vimetolewa na Madaktari rafiki wa Kampuni hiyo kutoka nchini Austaria na
vimegharimu Shilingi Milioni 54.
mwisho
No comments: