Mkuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesya akiongea katika kamati ya kupitisha azimio la jimbo jipya la uchanguzi mjini kahama.
WILAYA ya Kahama huenda ikapata Jimbo jipya la uchaguzi kutokana na kuonekana kuna mwingiliano na utata mkubwa katika usimamizi wa uchaguzi katika baadhi ya kata baada ya kugawanywa kwa Halmashuri tatu hivi karibuni ndani ya majimbo mawili ya uchaguzi.
Hayo yalibainishwa juzi na Mwenyekiti wa Baraza la ushauri la maendeleo ya Wilaya (DCC)ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya katika kikao cha baraza hilo kilichokaa juzi kujadili mapendekezo hayo ya kuanzishwa kwa jimbo la tatu.
Mpesya alisema kuwa kwa sasa katika Wilaya ya Kahama kuna jumla ya Halmashauri tatu yaani ile ya Msalala, Ushetu pamoja na Mji huku majimbo yakiwa ni mawili hali ambayo inaweza kuleta mkanganyiko katika usimamizi wa uchaguzi unaokuja hapo mwakani.
Katika kikao hicho baadhi ya wajumbe wake walipendekeza kuwepo kwa majimbo matatu yaani jimbo la Kahama, jimbo la Ushetu pamoja na jimbo la Msalala ambpo katika jimbo la kahama kuna idadi ya kata 20 zenye idadi ya wtu wapatao 258,457 na hivyo kufanya kukithi vigezo.
Pia waliendelea kupendekeza kuwepo pia na Jimbo la Ushetu ambalo litakuwa na jumla ya kata 19 na idadi ya watu wapatao 291,395 pmoja na jimbo la Msalala ambalo litakuwa na jumla ya kata 16 zenye idadi ya watu wapatao 267,548.
Katibu wa kikao hicho Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Isabela Chilumba alisema kuwa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi sura 343 kifungu namba saba (1) ambayo inamtambua Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya au Mji kuwa msimamizi wa uchaguzi katika jimbo, majimbo yaliopo kwa sasa yaani Jimbo la Kahama na Msalala yana mwingiliano mkubwa wa kiutawala jimbo moja maeneo ya kiutawala yakiwa katika halmashauri mbili.
Aidha Chilumba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu alisema kuwa tatizo jingine ni uwepo wa mwingiliano wa takwimu za wapiga kura katika halmshauri moja na nyingine hususani katika uandaaji wa daftari la wapiga kura kutokana mipaka ya kimajimbo na mipaka ya kihalmashauri.
Pia katika kikao hicho wajumbe walijadili mapendekezo ya kunazishwa kwa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kutokana na Mji huo kukidhi baadhi ya vigezo kama vile asilimia 30 ya shughuli za kiuchumi, kiwango cha huduma za hali ya juu.
Mwisho
No comments: