Mbunge wa jimbo la kahama Jemes Lembele akiongea na waandishi wa habari na kamati ya wilaya ya maendeleo Dcc katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa kahama juu ya utengwaji wa majimbo .
MBIO za
uongozi wa Wilaya ya Kahama kufanya jitihada za kutaka mji
huo kuwa Manispaa mpya hapo siku za baadaye huenda zikakwama kutokana na
makusanyo madogo ya mapato ya ndani yanayokusanywa na Halmashauri hiyo.
Mbunge wa Jimbo la
Kahama James Lembeli aliyasema hayo wakati akichangia mapendekezo ya kuanzishwa
kwa Halmashauri ya manispaa ya Kahama katika kikao cha kamati ya ushauri ya
maendeleo ya Wilaya ilifanyika hivi karibuni Mjini hapa.
Akisoma
mapendekezo hayo mbele ya Wajumbe wa kikao hicho Mkurugenzi wa Halmashuri ya
Mji wa Kahama Felix Kimaryo alisema kuwa wameamua kuleta mapendekezo hayo
katika kikao hicho kutokana na mji huo kukidhi baadhi ya vigezo vya kuwa
Manispaa.
Alisema kuwa
baadhi ya vigezo vinavyochangia Mji huo wa Kahama kuwa Manispaa ni pamoja na
kuwa na shughuli za kiuchumi kwa asilimia 30 za kibiashara na kuongeza kuwa
hiyo ni moja sifa inayofanya mji huo kukidhi vigezo hivyo.
Pia Mkurugenzi
huyo wa Halmashauri ya Mji alisema kuwa kiwango cha huduma za hali ya juu
pamoja na Halmashauri kujitegemea kwa asilimia 70 na kuongeza kuwa mapato ya
ndani yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku mfano 2012/2013 mapato yalikuwa ni
kiasi cha bilioni1.2, mwaka 2013/2014 yalikuwa kiasi cha shilingi billion 2.4.
Kimaryo alisema
kuwa katika mapato ya mwaka 2014/2015 mapato ya ndani yalikuwa ni billion 3.8
kiasi ambacho kilipingwa vikali na Mbunge wa Jimbo la Kahama James lembeli kwa
kusema kuwa kiasi hicho ni kidogo na kungeza kuwa ili Halmashauri ya Mji kuwa
manispaa lazima kuwe na uwezo wa kukusanya mapato ya ndani kiasi cha wastani wa
shilingi bilioni sita.
“Kuna kitu kimoja
Mkurugenzi hujakisema kahusu taarifa yako ambacho ni kiasi cha mapato ya ndani
ya Halmashauri yako ambayo ni madogo sana lakini mimi ninaunga mkono
mapendekezo ya kuanzishwa Halmashauri ya mpya ya Manispaa ya Kahama”, Alisema
James Lembeli Mbunge wa Jimbo la Kahama.
“Jitahidini katika
kukusanya mapato ya ndani mbona kuna vyanzo vingi tuu vya mapato ambavyo
watendaji wako hawatozi mfanao kodio za majengo, mabango pamoja na mambo
mengi tuu mkikusanya vizuri hata hicho kiwango cha serikali unaweza kukifikia
na kukipita”, Alisema Lembeli.
Aidha Mbunge huyo
alisema kuwa kwa sasa Mji wa Kahama unakuwa kwa kasi na ni moja kati ya
Halmashauri zilizochelewa kupandishwa hadhi lakini kwa hilo aliwataka viongozi
wa Halmashauri ya mji wa Kahama kukaa katika vikao vyao kungalia jinsi ya
kukusanya mapato ili kuweza kukidhi viwango hivyo.
mwisho
No comments: