Hivi ndiyo hali ilivyokuwa katika mji wa kahama wakati wa mandamano ya chadema ambapo jeshi la polisi limewenza kuzibithi madamano hayo .
Gari la polisi likiwa katika doria la kudhibiti mandamano hayo .
Hivi ndiyo wanachama wa chama cha maendeleo chadema katika ofisi yao.
Haya ndiyo mabango yalikuwa yameshikwa na wafasi wa chama hicho .
Hii ndiyo ofgisi ya chadema wilaya ya kahama .
Mmoja wa wanachama wa chadema Eng Thadeo jockimu mwenye suti nyeusi akiwa katika ofisi ya chama hicho baada ya kudhibitiwa kwa mandamano hayo.
Baadhi ya wafasi wa cha ma hicho wakiwa na mabango nyenye maneno ya kuikejeli serikali ya ccm kwa kutumia jeshi la polisi kwa kudhibiti madamano hayo .
Hivi ndiyo wafasi wa chama hicho wakiwa na mushangao wa kuzuhiwa kwa mandamano hayo leo mchana. .
Umati wa wanachama wa chadema wakiwa ofisini kwao wakitafakali hali ya kuzuiwa kwa madamano hayo. .
Jeshi la polisi wilayani kahama likiwatawanya baadhi ya wanachama wa chadema leo mchana katika barabara ya samanga.
Diwani wa viti maalumu wa chadema Winnefrida mwanula akiwa katika kituo cha polisi wilani kahama baada ya kukamatwa jeshi hilo kwa kuvunja amri halali ya jeshi la polisi .
Mwenyekiti wa chama cha maendeleo chadema juma Protes akiwa na baadhi ya madiwani wa chama hicho winnefrida mwenula mwenye kofia na Amosi sipemba wakiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi baada ya kukamatwa wakati wakihitisha kwa mandamano hayo.
Mwenyekiti wa chadema wilaya ya kahama juma Protes akiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi leo mchana baada ya jeshi hilo kudhibiti kwa mandamano hayo .
Baadhi ya wafasi wa chama hicho wakiwa nje ya ofisi hiyo .mwenye suti Eng Thadeo jockimu akiwa ameshika kitabaa cheupe kwa kuashilia Amani kwenye madamano hayo .
Haya ndiyo mabango yaliondikwa na wafasi wa chama hicho .
Na
Mohab Dominick,
Kahama,
Sept
24,2014.
JITIHADA
za Jeshi la Polisi nchini kudhibiti kwa amani maandamano yasiyo na
kikomo ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo kupinga kuendelea kwa bunge la
Katiba imeshindikana wilayani Kahama baada ya kuwatanya wafuasi wa chama hicho
kwa mabomu.
Maandamano
hayo ambayo yanaratibiwa nchi nzima na chama hicho ambapo maeneo mbalimbali
nchini yalishindikana kufanyika zaidi ya kuonekana Askari Polisi wakirandaranda
mitaani,wilayani Kahama chama hicho kimethubutu kuyafanya,na kulifanya Jeshi la
Polisi mkoa wa Shinyanga kuyadhibiti kwa kupiga mabomu ya machozi.
Katika
maandamano hayo ambayo kulikuwa na wafuasi wengi wa chama hicho waliokusanyika
katika ofisi za wilaya za chama hicho kuanzia saa moja asubuhi yakiongozwa na
Mwenyekiti wa Chama hicho Juma Protas na baadhi ya madiwani wa chama hicho
wakiwa wamejifunga vitambaa vyeupe mikononi mwao kuashiria amani.
Wafuasi
hao waliokuwa na mabango mbalimbali yanayolaani seriakali mabango hayo
miiongoni yakisomeka; “Serikali ya CCM inachofanya ni utapeli mtupu.Bunge la
Katiba ni mpango wa wizi mtupu ole wenu
2015.”pia “Kikwete ,Samweli 6 Ufedhuli wa kufuja fedha za Watanzania kwa kigezo
cha Bunge la Katiba acheni mara moja”na mengine kibao,walianza maandamano hayo
rasmi mnamo saa tatu asubuhi.
Wakiwa
katika maandamano ambayo yalitawaliwa na utulivu wakianzia katika ofisi zao za
chama wakiwa na vitambaa vyeupe walivyovaa kichwani na mikononi ghafla
ziliibuka gari nne za polisi zilizokuwa na askari zikiongozwa na PT
0841,walifika na kuwatawanya kwa mabomu ya machozi wafuasi hao,hatua ilileta
mparanganyiko mkubwa.
Aidha
baada ya Polisi hao kuwatawanya kwa mabomu wafuasi hao wa CHADEMA walifanikiwa
kuwatia mbaroni viongozi watatu wa Chama hicho ambao ni Mwenyekiti wa
wilaya,Juma Protas,Diwani wa Kata ya Nyihogo,Amosi Sipemba na Diwani viti
maalumu Winfrida Mwinula.
Hata
hivyo baada ya kukamatwa Mwenyekiti wa Chama hicho alisema Bunge la Katiba
kusimamishwa mara moja kinachofanyika Dodoma hakiwezi kupelekea kupata Katiba
ya Watanzania.
Alilaani
kitendo cha kukamatwa na polisi waliotumia nguvu kuwatawanya kwa silaha watu
ambao hawakuwa na silaha wala kuashiria uvunjifu wa amani,huku akisisitiza kuwa
serikali imepiga marufuku maandamano kwa ujumla wake lakini uongozi wa chama
chake wilaya uliandika barua ya kutoa taarifa kwa mujibu kanuni na sheria ya
vyama vya siasa.
“Katiba
inaturuhusu kutoa taarifa kwa mujibu wa sheria inavyoelekeza,hatua ambayo
tuliietekeleza lakini Jeshi la Polisi halikutoa majibu kama limeyazuia
maandamano hayo”,Alisema Protas.
Alisema
anashangazwa na Jeshi hilo kuleta askari wengi wakiwa za moto na mabomu ya
mchozi na magari manne jambo ambalo lingeweza kujibiwa kwa maombi ya barua
tuliyowapelekea.
Nae
Diwani wa Viti Maalumu Winifrida Mwinula alisema kuwa Bunge hilo linaendelea
kula fedha za wananchi jambo ambalo mbunge mmoja katika Bunge la Katiba
analipwa shilingi Laki saba kwa siku jambo ambalo mwananchi wa kawaida
anashindia mlo mmoja duni kwa siku huku wao wakiendelea kuneemeka huku wananchi
wa kawaida wakiwa na maisha duni.
Kwa
upande wake Diwani wa kata ya Nyihogo Amosi Sipemba alisema kuwa jambo la
maandamano lilpo kikatiba na Chadema wanachokiona katika Bunge la Katiba halina
manufaa kwa wananchi hasa kwakuwa linapindishwa pindishwa na kuona
kinachofanyika ni ufisadi mtupu.
Pia
mfuasi mmoja wa chama hicho Injinia Tadeo Joachimu alisema kuwa inashangaza
jeshi la polisi kuyaingilia wakati yapo Kikatiba,na kukilaani chama cha
mapinduzi kutumia dola kukiangamiza CHADEMA jambo ambalo alidai ukiukwaji wa
Katiba.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha alithibitisha kuyasambaratisha
maandamano ya chama hicho na kufanikiwa kuwatia mbaroni viongozi watatu wa
chama hicho kwa mahojiano zaidi.
MWISHO.
No comments: