Hii ndilo jengo la shule ya kadati kata ya isagehe wilayani kahama kama ilivyokutwa na waandishi wa habari .
Hili ndiyo Darasa la shule ya wanafunzi 302 wakiwa chini bila ya madawati ya kusomea katika shule hiyo ya kadati wilayani kahama na mbuge wa huko ni mh Ezekiel maige .
Hawa ni baadhi ya wanafunzi wa kike katika shule ya kadati kata ya isagehe wilayani kahama wakiwa katika mstari shuleni hapo .
hivi ndivyo ilivyo baada ya kuanguka na upepo wa mvua serikali tuone huruma hawa walimu wetu.
Hii ndiyo nyumba ya mwalimu kabla kuanguka.hivi ndiyo nyumba ya mwalimu kuu wanotoa vijana wetu kwenda vyuo vikuu vya tanzania.
hili ndiyo Darasa la tatu katika shule ya kadati wilayani kahama kata ya isagehe mkoani shinyanga .
Wanafunzi wakiwa darasani ndani shule yao tunatengemea kupata mawaziri hapa .
Na Mohab Dominck
Sept 14,2014
KAHAMA
Shule ya Msingi Kadati
iliyopo Kata ya Jana tarafa ya Isagehe Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
inakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa madarasa hali inayosababisha baadhi
ya wanafunzi kusomea nje chini ya mti na kusabaisha kusahaulika mara kwa mara.
Hayo yamesema na mwalimu
mkuu wa shule hiyo Salu Luhendeka wakati akizungumza na gazeti la nipashe
ambapo amesema shule hiyo ina jumla ya wanafuzi 302 kuanzia darasa la kwanza hadi la saba huku
madarasa yakiwa matano na madawati 48.
Amesema kati ya madarasa
hayo mawili yapo Katika hali mbaya zaidi ambapo hayana sakafu tangu yajengwe
mwaka 1999, huku utoro wawanafunzi ikiwa ni changamoto kubwa kwani wazazi
wamekuwa wakiwakataza watoto kwenda shule kwa lengo la kusaidia shughuli za
Nyumbani.
Aidha ameioba serikali kuzijali shule zilizopo pembezoni
kwa kuhakikisha huduma zinawafikia walimu na wanafunzi na si kupendelea shule
zilizopo katika maeneo ya karibu na mjini au sehemu ambapo miundombinu ya
barabara na huduma zingine zinapatikana.
Mwalimu salu ametoa wito kwa wazazi ambao pengine hawana mwamko
wa kuwahamasisha wanafunzi kwenda shuleni.
Nao badhi ya walimu wa shule
hiyo wametaja sababu zingine zinazochangia kuongezeka kwa utoro ni Nyakati za
masika ambapo njia mbalimbali zinazoelekea shuleni hujaa maji na kulazimika
shule hiyo kufungwa kwa muda ili kusubiri mito ikauke.
Mwalimu Salome Mwangosi
ameiomba serikali kuwasaidia kuimarisha huduma za miundombinu shuleni hapo
ikiwa ni pamoja na kuimarisha barabara ili kuwasaidia kufuata huduma zingine
katika kata jirani na sehemu zingine.
Kwa upande wake mwalimu
Grace Urasa amesema uhaba wa madarasa
unasabaisha wanafunzi wanaosomea nje ya madarasa kushindwa kuelewa vizuri na
kwamba wakati mwingine walimu wanashindwa kuwafundisha.
Hata hivyo amesema suala la
ukosefu wa barabara zinaunganisha kijiji
hicho kimekuwa ni chanzo kikubwa cha kukwamisha ufanisi ya kazi zao huku
wakihangaika kusafiri wakati wa masika kutokana na maji kutwama barabarani.
Shule ya Msingi Kadati ina
jumla ya walimu 9 huku nyumba ya mwalimu ipo moja ambayo ni ya kudumu na
zingine 8 ambazo si za kudumu zilijengwa na wananchi kwa lengo la walimu hao
wanaishi karibu na eneo la shule.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa shule hiyo Michael Nkunga amekiri kuwepo kwa
changamoto hizo licha ya uongozi wa bodi ya shule kuanza juhudi za kukabiliana
na changamoto hizo.
Nae mwanafunzi Agnes Charles
ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano katika shule hiyo akizungumza na nipashe
akiwa nyumbani amiomba serikali kuingilia kati suala la
wazazi kuwakataza wanafunzi kwenda shule kwa lengo la kusaidia shughuli za
nyumbani.
wanafunzi wa darasa la saba
nchini wamehitimu masomo yao ya msingi ambapo
halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga jumla ya wanafunzi 462 katika shule za
serikali 72 na binafsi 8.
Mitihani hiyo ambayo ilianza
jana nan kumalizika wiki ilipita katika mji wa kahama hali imeelezwa kuwa
shwari na hakuna tukio lolote baya lililojitokeza katika kusimamia mtihani huo.
Afisa elimu Msingi katika
halmashauri ya Mji wa Kahama Aluko Aluko Amezungumza na hali siyo kwa halmashauri ya mji wa kahama .
MWISHO
No comments: