Mkuu wa wilaya ya bukombe Amani mwenegoha akitoa ufafanuzi juu ya suala wahamiaji haramu katika wilaya yake amesema kuwa kuna baadhi ya watanzania wanatafuta vijana toka nchi jirani za rwanda na burundi kwenda tabora kwenye mashaba ya tumbaku .
Baadhi ya wahamiaji haramu wakiwa chini ya ulinzi
Baadhi ya wahamiaji haramu wakiwa ofisi za uhamiaji wilayani bukombe
Mkuu wa wilaya ya bukombe hakitoa ufafanuzi juu ya ulinzi shirikishi kwa jamii ofisini kwake wakati akiongea na wanahabari ofisini kwake .
Na Mohab
Dominick
Sept 14,2014
GEITA-BUKOMBE,
WARUNDI 19
wamekamatwa mjini Ushirombo Wilayani Bukombe mkoani Geita wakiwa kwenye gari
aina ya Hiace wakielekea Mkoani Tabora,
mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkuu
wa wilaya ya Bukombe Amani mwenegoha amewaeleza waandishi wa habari kuwa jeshi
la polisi likiwa kwenye msako maalumu kufuatia tukio la majambazi kuvamia kituo
cha polisi kisha kuua askali wawili na kupora siraha zaidi ya kumi yakiwemo
mabomu ya machozi.
Amesema mpaka
sasa wameshawakamata watanzania wawili ambao wanafanya biashara ya kuwaingiza
warundi kinyemela kwa kile walichodai kuwa wanaenda mkoani Tabora kwa ajili ya
kuwatumikisha kama vibarua kwenye mashamba ya Tumbaku.
Mwenegoha
amesema kuwa tabia hiyo ya kuwaingiza warundi ni hatari kwa Taifa kwani watu hao huwa si
wema kwani wanapoingia na kutumikishwa
kama manamba hawaoni shida lakini madhara yake huja baadae pindi wakizoea na
kusoma mazingira kwani wakimaliza shughuli za kilimo na mavuno hurudi kwao na kuwaleta wenzao kisha kuanza kazi ya uvamizi.
Mkuu huyo
amesema warundi hao kesho watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya kosa la kuingia nchini bila kibari na
watanzania hao wawili kwa kosa la
kuwaingiza watu kuja kuishi nchini bila ya kibari halali,
Aidha mkuu
huyo wa wilaya ametoa wito kwa wananchi waache tabia ya kwenda nchi jirani
kusaka vibarua na kuwaingiza nchini pia ametoa donge nono la shilingi laki moja
kwa yeyote atayetoa taarifa sahihi kumpata jangili, jambazi mwenye siraha na
wahamiaji haramu.
Mwisho
No comments: