Mwenge
Kahama
Walimu wa shule mbalimbali
za serikali nchini wametakiwa kutojiingiza katika masuala ya siasa na badala
yake wajikite katika kufundisha wanafunzi kwa kazi walioajiliwa ili kupata
taifa lenye wataalam wengi katika jamii.
Wito huo ulitolewa jana mjini Kahama mkoani Shinyanga na mmoja wa wakimbiza mwenge wa uhuru kitafa, Wito Jaston wakati akizungumza na wanachi wa mji wa Kahama katika viwanja wa CDT wakati wa kuupokea mwenge wa uhuru.
Jaston Alisema kwa sasa wimbi la walimu la kujihusisha na makundi ya siasa limeshamiri katika maeneo mbalimbali hapa nchini hali ambayo imesababisha hata wanafunzi kuwagawa katika makundi ya kisiasa.
Alisema makundi ya wanafunzi hasa vyuoni ambao wamekuwa wakifanya migomo na maandamano ni kutokana na walimu kufundisha siasa mbovu mashuleni kuliko kufundisha uraia wa nchi ili kila mmoja apate uelewa wa kutosha na kuondokana na dhana ya kufanya siasa chafu yenye lengo la kuharibu amani ya nchi.
Hata hivyo alisema serikali haiwezi kuwafumbia macho walimu wa namna hiyo na kwamba wakurugenzi watendaji katika halmashauri mbalimbali hawana buni kuwabaini na kuwachukulia hatua za kisheria walimu wanaojihusisha na siasa wakat wa kazi zao.
Aliwataka walimu hao kuacha ualimu na kujikita katika masuala ya siasa na si kuchanganya mambo mawili kwa wakati mmoja kwani ufanisi wa kazi zao unazidi kupungua na kusababisha kupata taifa ambalo halina wasomi welevu na wenye maadili mabovu ambayo hayaendani na matakwa ya nchi.
Pamoja na mambo mengine kiongozi huyo ameataka wanachi kutojihusisha na mandamano yanayotangazwa na baadhi ya viongozi wa siasa kwani hali hiyo itasababisha amani iliyoasisiwa na baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuvurugika na kuleta machafuko ndani ya nchi.
Alisema kwa sasa kinachotakiwa ni wananchi waliona sifa ya kupiga kujitokeza katika kuipigia kura rasmu ya tatu ya Katiba pindi zoezi hilo litakapoanza ili kupata katiba mpya itakayosaidia kupatikana kwa haki katika kila sekta na kwamba kura ndiyo itakayoamua na si kufanya mandamano.
Mwenge wa uhuru katika halmashauri ya mji wa Kahama umetembelea miradi 13 yenye thamani ya shilingi Bilioni 4.2 na oktoba 3 mwaka huu unakimbizwa katika halmashauri ya Msalala katika wilaya ya Kahama.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni Jitokeze kupiga kura ya Maoni , tupate Katiba mpya

.MWISHO
No comments: