Akiona cha moto baada ya kwenda kufanya ukahaba kwenye sikukuu ya christmas ajikuta akiwa tabani kwenye mti huku akiwa ana fahamu
MSICHANA mmoja aliyetambulika kwa
jina moja la Jenipher, anayedaiwa kujiuza katika maeneo ya Shivaz na Kaloleni
jijini Dar es salaam, amekutwa akiwa amepoteza fahamu kando ya barabara, katika
harakati za kujipatia chochote kipindi hiki cha sikukuu ya Krismasi na mwaka
mpya.
Akiwa pembeni ya barabara, Jenipher
anayeelezwa kuwa maarufu mjini hapa, anadaiwa kuwa siku hiyo alizidisha idadi
ya wanaume aliotoka nao, kwa ajili ya kujipatia kipato cha kutosha ili aweze
kuburudika vizuri wakati wa sikukuu ya Krismasi.
Baadhi ya mashuhuda wanaomfahamu
msichana huyo walisema kwamba katika kipindi cha wiki nzima iliyopita, alikuwa
akisaka wanaume kwa bidii na kwamba alikuwa tayari kwa ajili ya kutoa huduma
hiyo mahali popote.
“Unajua hapa kila mtu na mambo yake,
huyu Jenipher siku zote tupo naye ila wao huwa hawaendi kulipia gesti, ila
wanafanya ngono popote hata mtaroni, kwenye ukuta ilimradi huyo mwanaume yupo
tayari, ila usiku alizidiwa na wanaume na hakuwa amekula,’’ alisema mmoja wa
dada poa aliyekataa kutaja jina lake.
Mmoja wa wamiliki wa baa iliyo
maeneo hayo, aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema wasichana wengi
wanaojihusisha na biashara hiyo wamekuwa na tamaa kiasi cha kushindwa kujali
afya zao, kwani baadhi yao huacha hata kula chakula, badala yake, hunywa pombe
aina ya viroba.
Hadi tunatoweka eneo hilo, bado
binti huyo alikuwa yupo eneo hilo akiwa hajitambui.
No comments: