Baadhi ya watoto walizaliwa usiku wa mkesha wa chritsmas katika hospitali ya wilaya ya kahama .
JUMLA
ya watoto kumi na nane wamezaliwa usiku wa mkesha wa sikukuu ya Christmas
katika hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani shinyanga ambapo kati ya hao 10
niwakiume na wakike 8.
Akizungumza
mganga mfawidhi hospital ya wilaya ya
Kahama Dkr,Charles Rwaikeza,alisema kuwa jumla ya watoto kumi na nane
wamezaliwa usiku wa mkesha wa sikuku ya Christmas wote wakiwa wamezaliwa
salaama bila matatizo yoyote.
Alisema
kuwa alipokea takwimu za watoto waliozaliwa kutoka kwa wakunga waliokuwa zamu
ambapo ilikuwa jumla ya watoto kumi nane wamezaliwa wakiwa na afya njema ambapo
watoto wakike 8 pamoja na watoto wakiume walikuwa ni 10.
Hata
hivyo Rwaikeza amewataka wakinamama waepuke kujifungulia nyumbani badala yake
pindi wanapojihisi mabadiliko ya kimwili wakati wa ujauzito wawahi katika
hospital ama zahati zilizo karibu nao ili kupata matibu ikiwa ni njia mojawapo
ya kujifungua salaama.
Aliongeza
kuwa pindi wakimama wajawazito wanapokuwa hospitalini wakisubili wakati wa
kujifungua na kupata usumbufu kutoka kwa wauguzi wasisite kufika katika ofsi ya
mganga mfawidhi kwa lengo la kupatiwa ufumbuzi wa matatizo yanayokuwa
yamejitokeza kwa wauguzi wa zamu.
No comments: