MWANDISHI WA HABARI WILLIAM BUNDALA AKIWA NA MTOTO SALOME EDWARD HIVYO NDIVYO AMBAVYO MIGUU YAKE INAVYOONEKANA IKIWA IMEPOOZA.
Hospitali ya Misheni
Wilayani Sengerema mkoani Mwanza imepata lawama kutokana na kitendo chake cha
kumuongezea damu ambayo siyo kundi lake mtoto
aliyeafahamika kwa jina la Salome Pastory mwenye umri wa miaka mine.
Taarifa hizo
zimegundulika kufuatia baba wa mtoto huyo Edward Pastory kufika katika ofisi za
Kijukuu Blog zilizopo Mjini Kahama kwa lengo la kuomba msaada wa kuwekwa
mtandaoni ili apatiwe msaada.
Pastory alisema kuwa
mtoto wake alianza kuugua mafua na kichwa na alipoikishwa katika hospitali ya
mgodi wa Bulyanhulu iliyopo wilayani Kahama aliambiwa mtoto wake ana upungufu
wa damu na maji.
Kufuatia majibu hayo
Pastory akiwa na mke wake waliamliwa kwenda hospitali ya misheni iliyopo
Wilayani Sengerema ili awez kusaidiwa kuongezewa damu na kupatiwa matibabu
makubwa.
Inadaiwa kuwa mtoto
huyo ambaye alikuwa na damu ya Kundi 0 aliongezewa damu ya kundi A Hali
iliyopelekea kupooza viungo vyake vyoye vya mwili ikiwa ni pamoja na kuacha
kuona kabisa kwa miaka mitatu sasa.
Taaarifa za mtoto huyo
kuchanganyiwa damu zilitolewa na daktari ambaye hakufahamika jina katika
hospitali ya misheni ya Sengerema alipowaomba radhi wana familia wa mtoto huyo
kuwa walipitiwa na kujikuta wamefanya kosa hilo na kuwaomba watafute damu ya
kundi 0 ili wamuwekee tena mtoto huyo.
Baada ya tukio hilo
mama wa mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Yulitha Jeremiah aliamua kukimbia
na kumtelekeza mtoto huyo kwa baba yake hali iliyopelekea baba yake kumpeleka
mwanaye kwa bibi yake Mereciana Malele aishie katika kijiji cha Kishimba mkoani
Geita.
Kwa mujibu wa baba wa
mtoto huyo baada ya kuona tatizo linakuwa sugu aliamua kumpeleka mwanaye katika
hospitali ya rufaa ya Bugando ambapo aliambiwa atafute shilingi laki tano ili
mtoto wake aweze kukaa,kusimama na kushika vitu huku akiambiwa macho yake
yataendelea kutoona.
Kufuatia hali ya ukata
ya baba huyo aliamua kufika ofisi za mkuu wa wilaya ya Kahama na kuomba
kuandikiwa barua maalumu ya kuomba msaada kwa wasalimia wema.
Taarifa zilizopatikana
kufuatia barua hiyo hivi sasa Edward amefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi
laki moja na kwamba bado anahitaji laki nne ili kuweza kumsaidia mwanaye.
Kutokana na tatizo hilo
Edward ameamua kuweka namba zake hapa 0764-769868 ili kwa yeyote atakayeguswa
jambo hili aweze kumsaidia na kumpigia ili ampe habari kamili la tukio hili.
MATUKIO KATIKA PICHA:
BABA WA MTOTO HUYO KULIA AKIWA NA MTOTO WAKE.
AKICHEZA NA MTOTO WAKE
MWANDISHI AKIWA AMEMBEBA MTOTO SALOME
HAPA AKIJARIBU KUMSIMAMISHA LAKINI ILIKUWA NGUMU SANA.
MTOTO SALOME AKIWA AMELALA HAWEZI KUKAA WALA KUSIMAMA.
No comments: