Nembo ya jeshi la polisi
Baadhi ya askari wa kituo cha polisi wilayani kahama wakiwa katika barabara kuu ya maeneo ambayo yanasemekana kuwa na fujo katika sherehe hizi za sikuku wakiwa tayari kwa lolote lile.
Jeshi la polisi wilayani Kahama
mkoani Shinyanga limetoa wito kwa wananchi wilayani humo kutoa ushirikiano na
jeshi hilo kwa kutoa taarifa za uhaarifu ili kuimalisha ulinzi na usalama
kuelekea katika sikukuu za krismasi na mwaka mpya.
Mkuu wa kituo cha polisi wilayani
Kahama Elias Ulomi alisema kuwa wananchi wanawajibu wa kushirikiana na jeshi la
polisi katika kulinda amani na utulivu katika kipindi hiki cha msimu wa sikuu
za krismasi na mwaka mpya kwa kutoa taarifa ya vyanzo vyote vya uharifu
kama wizi na uporaji wa mali zao.
Ulomi amesema kua jeshi la polisi
wilayani humo limejipanga vyema kuhakikisha amani na utulivu kwa wananchi wake
kuelekea katika sikukuu hizo ambapo jeshi hilo limeweka mipango madhubuti ya
kuimalisha ulinzi na usalama hasa katika maeneo yote ya kumbi za starehe kama
baa,na klabu, ambapo kutakuwa na walinzi wakutosha kuanzia siku ya mkesha wa
krismasi na kuendela hadi sikuu ya mwaka mpya.
Ameongeza kuwa katika kipindi hiki
cha sikukuu kumekuwepo na matukio mbalimbali kama ajari za barabarani pamoja na
baadhi ya wananchi katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo kuvamiwa na kupolwa
malizao na hivyo kuwaomba wananchi wote kuwa waangalifu katika kipindi
hiki ili waweze kusheherekea sikukuu hizo kwa amani na utulivu.
“jeshi la polisi tumejipanga vizuri
na niwatoe hofu wananchi wote wilayani Kahama washeherekee kwa amani na
uhuru siku ya sikukuu kwani ulinzi utakuwepo wa kutosha katika maeneo
yote,nawatakia sikukuu njema na mungu awabariki”alisema Ulomi.
Sikukuu ya krisimasi huadhimishwa
Decemba 25 kila mwaka ambayo ni sikukuu ya kiimani kwa wakristo wote duniani
kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mwokozi Yesu kristo,hali kadharika sikukuu ya
mwaka mpya huadhimishwa januari mosi kila mwaka ikiwa ni mwanzo wa mwaka mpya .
mwisho
No comments: