Rais wa Jamhuri ya muungano
wa Tanzania Jakaya Kikwete akihutubia taifa la Tanzania kupitia wazee wa
mkoa wa Dar es salaam jioni hii
Prof. Anna Tibaijuka aliyeng'olewa uwaziri jioni hii nchini Tanzania.Unakumbuka wiki iliyopita Waziri Anna Tibaijuka alijitapa kuwa akijiuzulu hata Rais Kikwete atamshangaaa? Lakini cha ajabu leo Rais Kikwete amemtaka atoke kwenye nafasi hiyo ya Uwaziri na achaguliwe mtu mwingine.
Akiwa kama Mtumishi wa serikali
ambaye anatakiwa kufuata maadili ya Utumishi wa umma aliamua
kupokea kiasi kikubwa cha fedha huku akijua kimaadili kama mtumishi wa serikali
haitakiwi, Rais Dr. Jakaya Kikwete amesema hayo wakati akizungumza na
taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee
jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wa Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa Wiazara hiyo Eliackhim
Maswi amesema ameagiza uchunguzi ufanyika na katika muda wa siku mbili au
tatu hivi atapewa taarifa ya uchunguzi huo na kuchukua hatua stahiki.
Na Kwa upande wa Majaji wa Mahakama
Kuu waliotuhumiwa Rais Dr. Jakaya Kikwete amesema anamwachia Jaji Mkuu Mh. Jaji
Mohammed Chande Othman ili achukue hatua za kimaadili kutokana na taratibu za
kimahamama na mara baada ya kujiridhisha atapewa taarifa na Jaji mkuu na
kuchukua hatua.
No comments: