Askari wa jeshi la polisi
wakiwa eneo la hospitali ya wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
Mwili wa marehemu ukiwa
umewekwa sakafuni/kwenye korido kutokana na hospitali ya wilaya ya Mbogwe
kukosa mochwari.
Jeshi la polisi wilayani Mbogwe mkoani
Geita linashikilia mwalimu wa shule ya msingi Kasandalala wilayani humo Laideth
Constantine mwenye umri wa miaka 33 baada ya kumnyonga mwanae wa kiume mwenye
umri wa miaka 7 akiwa kwenye nyumba ya kulala wageni(Gesti).
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia
jana ambapo
kamanda wa jeshi la polisi mkoa
wa geita Joseph Konyo amesema tayari wanamshikilia mtuhumiwa baada ya vipimo
vya daktari kudhibitisha kuwa mtoto huyo kanyongwa.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo
wamesema mwalimu huyo amekuwa na mambo ya kushangaza jamii kwani wakati
mwingine anajifanya mlokole,mara anakuwa mkali na kugombana na kila mtu hasa
wakati akiwa shuleni.
“Tumekuwa tukimshangaa mwalimu
huyu,kuna wakati anakuwa mlokole,wakati mwingine anakuwa,mtaratibu sana,sisi
tunashangaa sana kutokea kwa tukio hili”,walisema.
Kwa upande wake mganga mkuu wa
hospitali ya wilaya ya Mbogwe mkoani Geita Cosmas Kilosa amesema vipimo
vinaonesha kuwa mtoto huyo amefariki dunia kwa kunyongwa.
No comments: