Baba askofu minde akitoa neno la kuimarisha amani nchini katika misa ya chrismas
Baba askofu minde akiwapa watoto baraka za chrismas na mwaka mpya
watoto wakipokea baraka kwa mshika mkono baba askofu
pokea baraka za bwana ndiyo maneno ya baba askofu minde kwa watoto
njoo kwangu mpate baraka za bwana wetu
Baba askofu akisikiliza neno la mungu
pokeni baraka za bwana wetu
IMEELEZWA
kuwa Amani Tanzania inataka kupotea Kutokana na watu kutomcha mungu na maadili
kuporomoka kwa baadhi ya viongozi wa siasa nchini kutaka kujilimbikizia mali
hasa kipindi cha uchaguzi unaoendelea hali ambayo inahatarisha Amani.
Hayo
yamesemwa jana Mhashamu Askofu mkuu wa Jimbo katoliki la Kahama,Rudovick Joseph
Minde katika maadhimisho ya siku ya Christmas katika mkesha wa misa Takatifu
uliofanyika katika Parokia Tarajiwa ya roho mtakatifu Majengo wilayani Kahama
mkoani Shinyanga.
Askofu
alisema Watanzani tunahali mbaya Kutokana na amani inataka kupotea katika taifa
hili ambapo inapotezwa na watu wachache wenye uchu na madaraka ambao wanalengo
la kujilimbikizia mali zisizokuwa na tija yoyote hasa kipindi hiki cha mpasuko
wa kisiasa.
Hata
hivyo Askofu Minde amekemea watu wanaoifanya sikukuu kuwa nidiyo siku ya nafasi
ya kufanyia maovu kuvuruga amani ama ndiyo sehemu ya mapambo,kula
vizuri,kutembea barabarani bali aliwaeleza kuwa maana ya Christimas ni tendo la
upendo wa juu mungu kumpenda mwanadamu.
Amewataka
waamini wa madhebu ya kikristo kuiombea Amani ya Tanzania kwa kufanya ibada
makanisani na kusema kuwa amani ikipotea hakuna mtu atakayeweza kuirudisha na
kusema kuwa ili kuondoa changamoto za kimaisha ni lazima wafanye yale yampendezayo
mungu nakuongeza amani ya familia ni kusali pamoja nakushirikishana mambo
mengi.
Amesema
kuwa maadhimisho haya hufanyika kila mwaka ambapo wakristo wengi ulimwenguni
huungana kwa pamoja kusherehekea siku hiyo muhimu kwa lengo moja la kuendelea kumshukuru
mwenyezi mungu
Mwisho
No comments: