sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » Brien Holden Vision yatoa msaada wa vifaa vya kupimia macho Wilaya ya Mkuranga na Kibaha

 
Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya  Brien Holden Vision Institute Eden Mahayo (Pwani.kushoto)akimkabidhi msaada wa sanduku la vifaa vya kupimia macho Kaimu Mkurugenzi wa  manispaa ya Mkuranga  Mbenjamin Majoya   kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi 122 za  Mkuranga  ambapo wanafunzi hao watapata huduma ya kupima na kutibiwa macho bure.hafa hiyo ilifanyika hivi wilayani mkuranga mkoa wa Pwan..


Afisa maendeleo ya jamii ya mji wa kibaha mkoa wa pwani akikabidhiwa na Mashine ya kupimia macho na   Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya  Brien Holden Vision Institute Eden Mahayo (kushoto)   wakati wa hafla ya kukabidhi wa msaada wa  vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4  kwa ajili ya kuwahudumia wanafunzi  wa Wilaya hiyo ya Kibaha ambao watanufaika na  huduma hiyo ya  upimaji  macho pamoja na  matibabu bure.


TAASISI isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision  imetoa msaada wa vifaa vya kupimia macho wa zaidi ya sh milioni 11.4 kwa Wilaya za Mkuranga  na Kibaha ziliyopo mkoani Pwani mwishoni mwa wiki. 

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa msada huo ,Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya hiyo  Benjamin Majoya alisema  msaada huo utasaidia  katika kupandisha  kiwango cha taaluma kwa wanafunzi  katika Wilaya  hiyo kutokana  na idadi ya watoro  darasani kupungua  kuanzia mwaka huu. 

Alisema kupungua kwa idadi ya wanafunzi watoro kutakwenda sambamba na kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi watakaojiunga na elimu yasekondari mwaka ujao.

Alibainisha kuwa  msaada huo unaojumuisha mashine zote za kupimia macho pamoja kutengenezea miwani  za aina mbalimbali  utasaidia kuondoa tatizo la uoni hafifu ambalo hapo awali wazazi walikuwa na imani potofu kwamba huenda watoto wao  wamerogwa . 

Akielezea ukubwa wa tatizo hilo ,alisema kuwa uoni hafifu umekuwa sababu ya mwanafunzi kutokufanya vizuri kitaaluma kutokana na kuugua mara kwa mara hivyo kusababisha utoro. 

“Tunaishukuru sana Taasisi ya BrienHolden Vision kwa msaada  waliotupatia na tunaahidi  kuutumia kwaajili ya wananchi ,na ifahamikie kwamba hii itabaki kuwa mali ya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga  ’”alihitimisha Majoya. 


Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya  Brien Holden Vision Institute Eden Mahayo (Pwani.kushoto)akimkabidhi msaada wa sanduku la vifaa vya kupimia macho Kaimu Mkurugenzi wa  manispaa ya Mkuranga  Mbenjamin Majoya   kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi 122 za  Mkuranga  ambapo wanafunzi hao watapata huduma ya kupima na kutibiwa macho bure.hafa hiyo ilifanyika hivi wilayani 002mkuranga mkoa wa Pwani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Eden  Mashayo alisema  lengo la Taasisi yake ni  kuwajengea uwezo wa kuona wanafunzi pamoja na walimu lakini pia kutoa mafunzo kwaajili ya walimu  ili waweze kuwapima wanafunzi  wapate huduma stahiki ili kuondokana na tatizo hilo.

Mashayo aliahidi ushirikiano baina ya  Taasisi yake ,Wizara ya Afya,Wilaya ya mkuranga  na kwa kuleta mtaalamu wa masuala ya macho kila mwezi mara mbili ambaye atakuwa akiwahudumia wakazi wa eneo hilo ili kuondokana na tatizo la uoni hafifu  ambalo litapungua kwa asilimia 10 . 

Kwa  upande wake Mkuu wa Mratibu wa  huduma za macho Taifa kutoka Wizara ya Afya Dk Nkundwe Mwakyusa alisema kuwa  mradi huo unaosaidia shule za Msingi  bagamoyo na Kibaha umeshahudumia  shule 121 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili utahudumia shule 116 . 

Akizungumzia  changamoto zinazowakabili alisema kuwa  huduma hizo hazipewi kipaumbele  kwasababu serikali inajua tu kunawafadhili . 

Hata hivyo alibainisha kuwa  ili kutatuua changamoto hizo  na kuifanya jamii iwe na uelewa sahihi juu ya magonjwa  ya macho mikakati iliyopo huenda mambo yakabadilika  na mwaka huu jamii itaanza kupata taarifa sahihi kuhusu magonjwa ya macho. 

Naye  daktari Mtalamu wa macho  Gilbert Massawe wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga na Afisa Maendeleo ya jamii mji wa kibaha Leah Rwanji waliishukuru Wizara ya Afya sambamba na Taasisi ya Brien Holden Vision   kwa msaada wao na kubainisha kuwa utasaidia kupunguza idadi ya utoro kwa wanafunzi kwa asilimia 10.

  

 .

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply