Wajumbe na wazazi wa serikali ya mtaa sokola wakiwa nje ya ofisi ya mwalimu mkuu shule ya msingi majengo .
Baadhi ya mwanafunzi wa shule ya msingi majengo wakiwa nje kwenye mapumziko .
Wanafunzi wa kike wakiwa chini ya mti katika shule ya msingi majengo.
Wajumbe wa kamati ya wazazi walitumwa na mwenyekiti wa mtaa kwenda kuongea na waziza juu ya ujenzi wa matundu ya vyoo kujenga masika .
Baadhi ya wazazi wakiwa nje ya jengo la shule ya msingi majengo.
Baadhi ya Tripu za mawe ambazo zimeletwa hapo shule kwa ajili ya ujenzi huo ambapo katika ujenzi huo zinatakiwa Tripu kumi na tano na wajumbe wa serekali ya mtaa kuona kuna jamaa za ubadilifu katika ujenzi huo .
Hapa ndiyo eneo ambalo linamjengwa matundu ya vyoo na upande wake wa kushoto kuna vyoo vya wanafunzi hao jambo ambalo wajumbe wa kamati ya serekali ya mtaa imesimamisha ujenzi huo kwa kipindi hiki cha masika na usalama wa watoto hapo shuleni .
Baadhi ya wajumbe wakiwa wamekaa juu ya mawe ya ujenzi wa matundu ya vyoo na mashimo wakitafakali juu ya ujenzi huo wakati wa kipindi cha masika wakati eneo hilo ni la kichanga .
Mjumbe wa serekali ya mtaa wa sokola kupitia chadema chancellas sumer akiongea na baadhi ya mwanachi na kamati yake juu ya ujenzi huo wa matundu ya vyoo katika shule hiyo .
Chancellas sumer akisisitiza jambo juu ya uhalibifu wa fedha za wananchi juu ya ujenzi wa matundu ya vyoo wakati wa kipindi cha masika shuleni hapo .
Baadhi ya wazazi wakiangalia eneo ambalo ujenzi wa matundu ya vyoo ambayo yanaotakiwa kujenga hapo wakati eneo hilo ni kichanga kwa kipindi cha masika ni kuhalibu fedha za umma .
Mwenyekiti wa mtaa wa sokola mary sumuni( Hali maarufu mama mchungaji ) kupitia chama cha maendeleo chadema akionyesha wazazi na wajumbe wa mtaa wa sokola juu ya ujenzi wa matundu ya vyoo eneo hilo.
KAHAMA,
Wajumbe
wa kamati ya serikali ya mtaa, wa sokola wilayani kahama mkoani shinyanga
wakataa ujenzi wa mashimo ya matundu ya choo kujengwa katika kipindi cha
masika katika shule ya msingi majengo.
Haliyoilibanika
wakati wa mwenyetiki wa mtaa wa sokola mary sumuni alipotembelea shuleni
hapo kujua kero za shule na kubaini ubadilifu wa ujenzi wa matundu ya choo na
kero kwa wazazi shuleni hapo .
Aidha
mwenyekiti huyo alisema kuwa shule hii imekuwa na mingongoro ya mara kwa mara
ya michango isiyokuwa na maelenzo ya kutosha toka kwa mwalimu mkuu wa shule ya
majengo,masula japhet .
Akielenzea
zaidi mwenyekiti huyo wa mtaa wa sokola alisema kuwa kwa kuwa sisi ni wajumbe
wapya wa serikali ya mtaa ni lazima kujua vitu vyetu katika serikali ikiwemo
shule hii na vitu vingine vinavyohusu jamii iliyopo hapa alisema sumuni.
Tulikumbaliana
mashimo hayo ya choo yatakuwa na gharama ya shilingi laki sita,mawe tripu kumi
,au kumi na tano ,mchanga aidha mwenyekiti alisema kuwa shughuli hiyo yote
inaghalimu kiasi cha shilingi milioni 6 michango ya wananchi wa kata ya majengo
mtaa wa sokola.
“Hebu
fikiria huu ujenzi gani wa wakati wa masika si nikupotenza fedha za wananchi
hebu ona hapa kuna mawe tripu 3 za mawe wakati tulikumbalia tripu 10 mpaka 15
na eneo hili lina chemu chemu hebu ona haya maji yanavyotoka huu ni ubadilifu
wa fedha za umma alisema mary sumuni”
Aidha
mama moja Naomi mussa ambaye alipeleka shule motto wake alitozwa ada ya
kuandikishwa kwa shule motto kiasi cha shilingi elfu ishirini na sita na
alisema mimi sina kwa sasa ila nitalipa kidongo kidongo mwalimu alikata na
kunifukunza eneo la shule na kusema chukua motto wako hapa kama una hela hizo.
“wewe
hunakwenda kwa mwenyekiti wa mtaa hapa hunaleta mambo ya sias shule na mambo ya
sias wapi na wapi,tuone sasa tena kama natawenza kukusaindi hii barua mimi
siongopi wala huyo siyo mkuu wa kazi wewe toka nje hapo”Alisema mwalimu mkuu.
Aidha
afisa Elimu wa halmashauri ya mji wa kahama Aluko Lukolela alipotafutwa
kwa njia ya simu yake ya mkononi kuhusu suala hili alisema habari
hizi nimezipata toka kwa mwenyekiti wa mtaa wa sokola mary sumuni juu ya
ujenzi wa mashimo ya choo na matundu hayo.
Akifafanua
zaidi kwa njia ya simu nyenye aliomba tuwasiliane ofisi kwake nipashe ilikwenda
ofisi na kukaa hapo bila kuoneka ili awenze kuzumgumuzi suala kwa muda wa siku
mbili bila ya mafanikio.
Nipashe
ilifika eneo la shule ya msingi majengo kuona hali hiyo ya ujenzi wa matundu na
vyoo vya shule ilikupata ukweli kwa mwalimu mkuu na nyenye hakuwa tayari
kuongelea suala hilo niendi kuona na afisa elimu ndiyo msemaji wa shule hiyo .
Aidha
nipashe ilijione uchimbaji wa shimo hilo na kusitishwa kwa ujenzi huu toka kwa
mwenyekiti wa mtaa huo wa sokola mary sumuni mpaka kiangazi mwaka huu ndiyo
ujenzi huo uendelea kwa kuwa hiki ni kipindi cha masika alisema mwenyekiti huyo
mary sumuni .
Mwisho.
No comments: