sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » WALIMU KATENTE SHULE YA MSINGI WAWAFURAHISHA WATOTO YATIMA 99-BUKOMBE.



Rai hiyo aliitoa jana mwalimu mkuu wa shule ya msingi Katente
kemilembe Grigory  iliyoko eneo la machimbo ya madini ya dhahabu
umbali wa kilometa moja kutoka mjini Ushirombo wilayani Bukombe.
Mwl Kemilembe alisema

 “naiomba jamii iige mfano wetu wakuifanya siku ya wapendanao ambayo imepita tangu februari 14 lakini sisi tumeamua tuienzi leo huku tukisherehekea na watoto yatima hawa 99 na  wale wanaoishi katika mazingira magumu kwenye ukumbi huu wa sun rise”

Kemilembe Alisema sanjari na sherehe pia yeye akishirikiana na walimu
wenzake walipata maono ya kuwaalika watu ili nao wakaone umuhimu na mahitaji ya watoto hawa ambao hawana wazazi wao wote wengine
walifariki kwa kupondwa na vifusi kwenye machimbo na wengine wazazi wao walifariki kwa magonjwa kama vile Ukimwi, kansa ya shingo ya kizazi, sukari na shinikizo la damu na ajari.

Alisema “tukibadiri fikra zetu watanzania kwenye siku ya wapendanao
tuliyoizoea ambayo huwatunaifanya mara moja kwa mwaka na tukaelekeza mawazo yetu kuwapenda watoto yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu kwa kusherehekea nao huku tukijitolea michango ya hali na mali ili kuwasaidia mahitaji muhimu  hakika watoto hawa wakitanzania
hawatakuwa wakiwa hivyo wataishi ,watakuwa na kusoma bila ya kuwa na msongo wa mawazo kuwa baada ya wazazi wao kutoweka jamii ipo”alisema mwl kwmilembe Kwa upande wake mwl wa malezi shuleni hapo Savera  Mugisha aliwaeleza wageni waalikwa kwenye hafla hiyo kuwa watoto walionao yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu ni wengi wapatao 99 lakini wanamahitaji mengi kama vile viatu ,sale za shule ,sabuni na mambo muhimu.

Mwl savera alisema kuwa kwa upande wa watoto wa kike ambao wamevunja ungo shule yao ina chumba mbadala cha kuwasaidia na kuwaelimishia hao watoto yatima kujisetili na hali hiyo hali ambayo vitendea kazi vinahitajika ili waweze kujisikia vizuri na kuendelea na masomo yao vyema.

Hivyo mwl Savera aliwaomba waalikwa wachangie kwa hali na mali ili
watoto hao waweze kupata mahitaji hayo yakuweza kutumia kipindi cha
mwaka mmoja.

Aidha baadhi ya watoto hao yatima wanaosoma shule ya msingi katente
ambao ni Kasanda Lifa ,(14) Husna Hussein (13) Abal Leonard (12) na
Rehema Daud (13) kwa niaba ya wenzao 99 wamefurahishwa na mpango wa walimu wao wa kuwafanyia sherehe kama hiyo ya wapendanao huku walimu wao wakiwaandalia chakula na vnywaji sanjari na kuwapa zawadi.

Hivyo mwanafunzi Rehema Daud alisema kuwa wamejisikia kuwa jamii
inawathamini na walimu wao wanawapenda kwani wamepata zawadi za sare za shule viatu ,madaftari na kalamu sambamba na sabuni hivyo kwaniaba ya watoto wote yatima anawaombea kwa mwenyezi mungu awajalie na wazidi kuwakumbuka pia anawaomba mashirika kama vile Redcross mwaka jana waliwapa viatu vya Raba vyeusi lakini kwa sasa vimeisha hivyo anawaomba mashirika mengine nchini yawatembelee ili waende wakaone maisha waliyonayo shuleni hapo.

MWISHO



«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply