sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » DC .KAHAMA ATUMIWA KUCHUKUA MIFUKO 300. YA SARUJI BULYAHUNULU MADIWANI

 Diwani wa kata ya Bulyahunulu joseph makoba akisisitiza jambo juu ya mifuko mia tatu ya saruji iliotolewa na mgodi wa bulyahunulu kwa ajili ya ujenzi wa mahabara ya shule ya sekondary Bulyahunulu ambayo mkuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesya alipokea toka mgodi huu .
 Diwani wa kata ya Bulinge meneja Nugi akisiliza hoja ya mifuko ya saruji iliotolewa na diwani wa viti maalum asha Binde kwenye kikao cha madiwani cha kawainda katika ukumbi wa Halmashauri hiyo .
 Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya msalala wakisikiliza kwa umakini hoja ya diwani wa viti maalum juu ya sakata la madiwani juu ya mifuko ya saruji alichukua mkuu wa wilaya ya kahama toka mgodi wa Bulyahunulu .
 Baadhi ya wakuu wa idara mbalim mbali wa Halmashauri ya msalala wakiwa katika kikao cha kawaida cha halmashauri hiyo .
 Wakuu wa idara mwenye miwani ni kati ni Dr Hamadi Nyembea wakisikiliza hoja katika kikao cha madiwani .
 Mkurungezi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala  Patrick  karangwa akijaribu kuweka mambo sawa juu ya sakata la madiwani wa kata ya Bulyahunulu juu ya mifuko ya saruji mia tatu iliyotolewa na mgodi huu katika kata ya Bulyahunulu kwa ajili ya ujenzi wa mahabara ya shule hiyo .
 Diwani wa kata ya isaka Ibrahimu msanja akisisitiza mifuko hiyo ya saruji kurundishwa kwa wananchi.
 Diwani wa Viti maalum Asha Binde aliotoa hoja ya mifuko ya saruji mia tatu ilichukuliwa na mkuu wa wilaya ya kahama.
 Baadhi ya madiwani wakiwa kwenye kikao wakisikiliza hoja zinazoendelea kwenye kikao hicho .
 Baadhi ya madiwani wa chadema walioibuha hoja ya mifuko ya saruji ya mifuko mia tatu .
 Diwani wa chadema Asha Binde na Mh Jaqline Nyamoko wakijadiliana juu ya sakata la mifuko ya saruji ilitolewa na mgodi wa Bulyahunulu .
 Mkuu wa Wilaya ya kahama Benson Mpesya akiwa ofisi kwake akiongea juu ya sakata la mifuko hiyo ya saruji na kusema kuwa nyinyi aliomba mifuko hiyo na nilipewa mimi .
Mkurungezi Mtendaji wa Halmashauri ya msalala Patrick kurangwa akiongea baada ya kikao cha baraza la madiwani juu ya sakata la mifuko mia tatu ya saruji alipewa mkuu wetu wa wilaya ya kahama .

 KAHAMA. 

Baraza la madiwani la halmashauri ya msalala wilayani kahama mkoani shinyanga limemuomba mkuu wa wilaya ya kahama Benson mpesya kurundisha mifuko 300 ya saruji ilitolewa na mgodi wa dhahabu wa Bulyahunul (ACACIA ) katika shule ya sekondary ya bulyahunul ilitolewa kwa ajili ya ujenzi wa mahabara.

Hayo yamesemwa kwenye kikao cha baraza la madiwani cha kawaida  juu ya mipango ya maendeleo ya halmashauri ya msalala na kuweka mikakati yake ya maendeleo.

Aidha Diwani wa kata ya Bulyahulu Joseph makoba akiongea katika kikao hicho alisema kuwa kwenye mahafari ya shule ya sekondary ya Bulyahunul waliomba msaada kwa mgeni rasmi ambaye ni afisa mahusiano wa mgodi wa ujenzi wa mahabara ya shule hiyo.

Diwani makoba aliendelea kufafanua kuwa baada ya risala ya shule waliomba ujenzi wa mahabara ndipo mgodi huliandi kutoa mifuko mia tatu (300)ya saruji kwa ajili ya mahabara hiyo.

“sisi kama viongozi tulisikia kuwa mkuu wa wilaya Benson mpesya kuwa imepewa mifuko mia tatu ya saruji ambayo shule na kata ya bulyahunul iliomba kwa mgeni rasmi ambaye ni meneja mahusiano Abdala msika na kupewa mifuko hiyo ”

Akifafanua zaidi DIwani huyo alisema kuwa sisi mifuko hiyo ya saruji bado hatujaiona katika kata yetu nab ado tunaendelea kuomba jambo ambalo limekuwa ni kero kwa mwanachi kwa kuwa tuliwambia kila kaya kuchanguia kiasi cha (shilingi elfu 30)Kwa kila kaya na kutoa kiasi cha shilingi elfu kumi na hizo zilizobakia ni kwa ajili ya mgodi kupunguza gharama kwa wanachi wetu .

“kwa maana hiyo mpaka sasa hiyo saruji inasemekana kuwa ilipelekwa kwenye bank ya matofari ya wilaya ya kahama jambo ambalo wanachi wa kata ya bulyahunul wamelipiga ”

Naye kwa upande wake Diwani wa viti maalum kupitia chadema Asha Bide kuwa ndiye alitoa hoja ya kutaka kujua mifuko mia tatu ya saruji iko wapi, tuliopewa na mgodi wa Bulyahulu,katika kikao cha baraza la madiwani.

Aliendelea kueleza kuwa mimi baada ya kubaini kuwa mifuko hiyo imechukuliwa na mkuu wa wilaya ya kahama na kwenda kwenye bank ya matofari na kutumika kwenda kwenye kata zingine jambo ambalo kata ya Bulyahunulu iliumiza kichwa kuomba msaada huo na kuambiwa kuwa tumesaidia kata za bulinge na Ngaya ambapo sisi tuliomba.

Pia kwa upande mwingine mkuu wa wilaya alinifokea na kuniambia mimi nimemuta mwizi katika sherehe ya kukaribisha mwaka nilipo taka ngusa galas yake alifokea sana na kusema mimi mwizi hunaweza kungongeana galas alisema Diwani huyo kwa machungu sana wakati akiongea na nipashe.
Naye Mkurungezi wa Halmashauri ya msalala Patrick kurangwa alikili kweli mifuko hiyo ilipokeliwa na mkuu wetu wa wilaya na hakuna na nia mbaya.

‘ ukweli wa jambo hili ni mkuu alipokea na kwa kuwa na halmashauri tatu aliona ni vema kupeleka kwenye bank ya matofari na kuona kusaindi kata hizo za Ngaya na Bulinge kwa manufa ya wote”alisema Patrick kurangwa .

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesya alipotafutwa kwake ofisini akuwenza kupatikana na kwa simu yake ya kingajani alipatina na kusema nipo nje ya wilaya labda tuwasiliane jumatatu 

Mwisho
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply