Hizi ni baadhi ya Risasi ambazo zimekamatwa katika mkoa wa shinyanga jeshi la polisi likishirikiana na wananchi kwa pamoja .
kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga justus kamugisha akionyesha baadhi ya siraha zilikamatwa mkoa wa shinyanga picha hizi na makitaba yetu .
KAHAMA .
Mkazi wa mulubona wilaya ya kasulu Saidi maulidi miaka 35
mkulima na mkazi wa kijiji cha mulubona Akamatwa na risasi 166akiwa na risasi
hizo na bunduki aina G3LMG pamoja na makoti mawili .
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Busoka wilayani kahama mkoani shinyanga jana majira
ya jioni,akiwa anatokea mkoa wa kigoma kuelekea mkoa wa singida.
Kwa mujibu wa
mashuhunda wa tukio hilo walisema kuwa jambazi hilo likuwa kwenye basi
la abiri lilokuwa na jina la bariadi Express ambapo basi ilikuwa likitokea
mkoani kigoma na askari wa doria wa task force ndiyo walipewa taarifa hiyo na
kulisimamisha basi hilo.
Aidha kwa mujibu wa shuhunda huyo john Charles alisema kuwa
hivi karibuni kumekuwa na mwinbi kubwa la majambazi kupita jioni na mabasi
yanayotoka mkoa wa kigoma na Geita na wilaya zake kumekuwa na matukio yaaaina
hiyo ya kila mara alisema john.
Aidha kwa upande wake kamanda wa polisi wa mkoa wa shinyanga
Justus Kamingisha alipoongea na gazeti la nipashe alisema kuwa jambazi hilo
likuwa kwenya Basi la Bariadi Express aina ya scania lenye namba T186
BFY.Ambalo jambazi hilo likuwe limepanda.
Kamanda wa polisi mkoani alizidi kusema kuwa jambazi hilo
likuwa vitu vingine kama vile ,makoti mawili ambayo yanafanana makoti ya
kipolisi jambo ambalo polisi waliokuwa doria na task force waliweza kumdhibiti
jambazi hilo na kulikamata .
Kamungisha alizidi kusema kuwa naomba abiria na raia wema
kuwa na hushirikiano na jeshi la polisi kwa kutoa tarifa kwani kujiokoa wote
watanzani ana siyo kwa mtu moja ni kwa taifa na wanachi na mali zao pia ni
wajibu wa kila mwanachi kutumia nafasi ya kutoa tarifa.
Kamanda Justus amesema kuwa jeshi hilo la polisi lina
mshikiri mhutumiwa huyo na ikikamilika uchunguzi wa tukio hilo hatafikishwa
mahakani kujibu tuhuma hizo za kukutwa na bunduki na Risasi hizo.
Mwisho
No comments: