IGP Ernest mangu akitoa salamu za mwisho kwa askari polisi aliyeuwa .
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime (SACP) amefafanua kuhusu kilichomsibu mtuhumiwa
wa mauaji ya askari polisi Joseph Isack Swai.
Kamanda
huyo alisema kwamba baada ya mauaji ya askari huyo, wananchi walikusanyika na
kuanza kumsaka mtuhumiwa Tissi Siril malya na majira ya saa tano usiku
walimkuta maeneo ya Mti Mkavu maili mbili mkoani Dodoma.
Alisema
kwamba wananchi walimkuta mtuhumiwa na panga alilotumia kumuua askari na kuanza
kumshambulia.
Pamoja
na Polisi kuwahi kufika eneo la tukio na kumchukua kumkimbiza Hospitali ya Mkoa
lakini daktari akagundua ameshafariki.
Aidha
Kamanda Misemi amesema mtuhumiwa huyo katika kumbukumbu tulizonazo ni kwamba
mwaka 2006 aliwahi kufungwa miaka mitatu (3) kwa kosa la kujeruhi, Pia mwaka
2009 alifungwa tena miezi sita (6) kwa kosa la kutishia kuua.
Aidha
pamoja na kutoa pongezi kwa wananchi kwa kuonyesha kuchukizwa na kitendo
alichomtendea Askari ,lakini amewataka kuacha kujichukulia sheria mkononi.
Pia
ametoa wito kwa wananchi tuanze kuchukua hatua kurekebisha maadili kuanzia
ngazi ya familia kwani tumeelezwa kuwa mtuhumiwa alikuwa ni mvutaji bangi kiasi
kwamba ilimfanya awe anafanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadili na sheria
za nchi.
Wakati huo huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest
Mangu aliongoza mamia ya wakazi wa Dodoma kumuaga Askapo Polisi aliyeuawa
wakati akitekeleza majukumu yake na na kuliagiza Jeshi la polisi kuongeza kasi ya
kupambanana uhalifu na wahalifu.
Askari huyo aliyeuawa
Koplo Joseph Swai (27) tayari amesafirishwa kwendaArusha kwa mazishi.
IGP Mangu alisema Jeshi
la polisi linatakiwa kuongeza kasi ya kupambana nauhalifu kutokana na
kuongezeka kwa vitendo hivyo ndani ya jamii.
“Kijana amekufa kishujaa
wakati akitetea mtu asiye na uwezo wakatiakinyanyaswa, katika kifo hiki askari
wapate cha kujifunza kwani kimewatianguvu na kuwawezesha kufahamu namna ya kukabiliana
na uhalifu.
Alisema msiba huo ni
fursa ya kujihami na kukomesha uhalifu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma. Chiku Gallawa alisema ni wajibu wa jamiikufichua wahalifu ili waweze
kukabiliana na mikono ya sheria.
Mbunge wa viti maalum Moza
Abeid aliitaka jamii kufichua waovu
kwani wako kwenye familia na wanajulikana na iwapo
wangekuwa wakitajwa ni vizuri kuliko kuachwa mpaka
wanapoleta madhara makubwa kwa jamii.
Akimwakilisha kamanda wa
polisi Mkoa wa Dodoma, kamishna msaidizi wa
Polisi, Emmanuel Lukula
alizitaka familia kulea watoto wao katika njia ya
kukataa uhalifu.
Mwisho
No comments: