Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda akiwa katika ibada ya
maziko ya Askofu Mstaafu wa Jimbo la Tunduru/ Masasi, Magnus
Mwalunyungu yaliyofanyia kwenye
kanisa la Tosamaganga
mkoani
Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda akizungumza na Rais wa Baraza la
Maaskofu Katoliki
Tanzania, na Askofu wa Jimbo la Iringa, Mhashamu Ngallekumtwa (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Aina
Masenza baada ya
mazishi ya Askofu Mstaafu
wa Jimbo la Tunduru Masasi, Mhashamu Magnus Mwalunyungu yaliyofanyika
kwenye Kanisa la Tosamaganga mkoani Iringa
.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda
amewataka Watanzania wasikilize na kufuata mafundisho yanayotolewa na viongozi
wa dini ili Tanzania iwe nchi yenye watu waadilifu na wenye hofu ya Mungu.
Ametoa wito huo leo mchana
wakati akizungumza na maelfu ya waumini na wananchi waliohudhuria ibada ya
mazishi ya Askofu Mstaafu Magnus Mwalunyungu kwenye kanisa la Moyo Mtakatifu wa
Yesu la Tosamaganga, Jimbo Katoliki la Iringa.
“Leo ni siku ya pekee ya
kuwasikiliza viongozi wa dini wakituasa tujiandae kwa maisha baada ya kifo.
Tukio hili la leo litupe nguvu ya kukubali kwamba kifo kipo licha ya kuwa
hakizoeleki na kinapotokea
kinaleta simanzi kubwa,”
alisema.
“Ninawasihi Watanzania
wote tufuate mafundisho yanayotolewa na viongozi wa dini zetu ili Tanzania iwe
na kundi la watu wenye hofu ya Mungu, waadilifu na wanyofu kama ambavyo
mahubiri ya leo
yamesisisitiza,” alisema.
|
ya Afrika Mashariki.
Akitoa mahubiri kwenye
ibada hiyo, Askofu Damian Dallu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea alisema
wanadamu wanahangaika na kuogopa kifo kwa sababu hawajui baada ya kifo maisha
yao yatakuwaje.
“Askofu Mwalunyungu
ameishi kwa miaka 85 na kati ya hiyo, miaka 55 alikuwa akitumikia kama padre na
kwa miaka 22 alimtumikia Mungu akiwa Askofu. Na hata baada ya kustaafu aliomba
awe Paroko pale Kidamalai ambako alitumikia kwa miaka minne. Maisha yake
yanaendana na neno kutoka kitabu cha hekima kwamba kifo cha mwadilifu ni
kupumzika kwa starehe,” alisema.
Ibada hiyo ya mazishi
ilihudhuriwa na Maaskofu wa kanisa katoliki zaidi ya 20.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, FEBRUARI 20,
2015.
No comments: