Kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga Justus kamungisha akitoa maelenzo kwa waandishi wa habari juu ya mganga wa kienyeji kutwa na buduki na risasi nane mji kahama .
KAHAMA ,
Jeshi la polisi mkoa wa
Shinyanga linamshikilia mganga wa kienyeji Zacharia Ngobeko Dogo(35),mkazi wa
kijiji cha Mbulu kata ya Mhongolo wilayani Kahama kwa kosa la kukutwa na
bunduki aina ya SMG yenye namba 8945 iliyotumika katika mauaji
ya Mary Kashindye aliyeuawa kwa kupigwa risasi hivi karibuni
wilayani Kahama.
Kamanda wa polisi mkoa wa
Shinyanga SACP Justus Kamugisha amesema mganga huyo wa kienyeji alikamatwa
akiwa na silaha hiyo ikiwa na risasi nane ndani ya magazine iliyokuwa
imehifadhiwa nyumbani kwake tarehe 18 mwezi wa pili mwaka huu saa saba mchana.
Kamanda Kamugisha amesema
mganga huyo na wenzake wawili wanatuhumiwa kuhusika katika matukio ya mauaji
yaliyotokea tarehe 8 mwezi huu saa tatu usiku kwa kumuua Mary Kashindye kwa
kumpiga risasi kutokana na ugomvi wa kiwanja kati ya marehemu na Jumanne Maige.
Amesema kutokana na
ugomvi huo aliwakodi Andrew Buteye Mtakatifu(38) mkazi wa Tabora na Daudi
Luchemela Ngasa(40) mkazi wa Nzega Tabora kutekeleza mauaji hayo.
Ameongeza kuwa silaha
hiyo pia ilitumika katika unyang’anyi wa kutumia silaha wa tarehe 13 mwezi huu
saa mbili usiku wilayani Kahama ambapo walipora shilingi milioni moja na nusu
dukani kwa Manyangu Mboje.
Kamanda Kamugisha
ameeleza kuwa katika mahojiano na watuhumiwa,wamekiri kuhusika katika matukio
yote mawili na kuhifadhi silaha kwa mganga huyo wa kienyeji.
Katika hatua nyingine
amesema watuhumiwa wamekiri kutenda makosa ya unyang’anyi kwa kutumia silaha
katika mkoa wa Mbeya,Mwanza na Tabora.
Mwisho
No comments: