sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » BUKOMBE. TFDA YAFUNGA MACHINJIO ZOTE WILAYANI BUKOMBE.KWA UCHAFU.

BUKOMBE. TFDA YAFUNGA MACHINJIO ZOTE WILAYANI BUKOMBE.KWA UCHAFU.
MAMLAKA ya Chakula vipodozi na dawa TFDA kanda ya Ziwa  imefunga
machinjio zote Wilayani Bukombe  Mkoani Geita  baada ya kufanya
ukaguzi wa kushtukiza na kukuta machinjio hizo  ni chafu zikiwa
zimezagaa funza ,siafu na hazina mitaro ya kutiririshia damu,na hazina
uzio.
Kwa muujibu wake mkaguzi mwandamizi TFDA kanda ya ziwa Julius Panga
amewaeleza wandishi wa habari kuwa hali walioikuta kwenye machinjio
hizo inatisha nan i hatari kwa maisha ya watumiaji yaani walaji wa
nyama katika wilaya ya Bukombe .
Panga amesema kuwa  wananchi wa Bukombe na vitongoji vyake wamo
hatarini ama tayari wengine wamekuwa wakiugua magonjwa ya mfumo wa
chakula na huenda hawajui chanzo cha tatizo ni nini kutokana na uelewa
duni juu ya usafi ya nyama katika machinjio na kwenye maduka yaani
bucha na magari ya kusafirishia nyama kutoka kwenye machinjio hadi
kwenye maduka ya kuuzia nyama.
Amesma wamefunga machinjio zote za Runzewe,Ushirombo ,katente namba
moja na zinginezo ambazo wamezikuta si Rasmi yaani machinjio Bubu kwa
muda usiojulikana hadi hapo mkurugenzi wa halmashauri atakapokarabati
na kuweka miundo mbinu mpya na bora vinginevyo wao kama wadhibiti wa
ubora wa vyakula kamwe hawata kubari wanajamii waangamie hivihivi
hivyo wanawaomba wananchi wavumilie kwa kipindi hiki kigumu cha kukosa
huduma hii ya kitoweo ama ukosajiwa nyama.
Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa wachinja nyama wilayani Bukombe
Amidulah Jumanne na wenzake Hamza Pius na Paul Jackson wameipongeza
mamlaka hiyo kwa uamuzi huo waliouchukua wakufunga machinjio kutokana
na kukithiri kwa uchafu hali ambayo wamesema wamekuwa wakiipigia
kelele muda mrefu na hata ilifika mahala wakachukua hatua ya kugoma
kuchinja hali ambayo iliwagharimu pale wananchi walipopiga kelele kwa
kukosa kitoweo.
Amidulah amesema mgomo huo ulidumu siku mbili wakasitisha na ndipo
walipo kwenda kumuona Afisa mifugo wilaya George Sabuni akawaeleza
kuwa tayari wamesha mpa barua Mkurugenzi na injinia tayari amesha
ainisha gharama za ukarabati machinjio ya mwalo ambayo gharama zake ni
kiasi cha shilini milioni 4.
Amesema maneno hayo yaliwaridhisha lakini hayakuzaa matunda kwani
ahadi hiyo ilikuwa mwaka jana mwezi novemaba, lakini hawakukata tama
mwezi januari mwaka huu walienda tena kumuona mkurugenzi ofisini kwake
akawaambi kuwa tatizo hilo amnalinjua lakini tatizo  halmashauri haina
pesa  ,hivyo akawaahidi kuwa wasubiri wakusanye fedha za malipo ya
pango la vibanda vyote vinavyozunguka soko ambavyo hulipwa kiasi cha
shilingi elfu hamsini kwa kila kibanda ambayo viko vibanda zaidi 200.
Hivyo ni vya soko kuu la ushirombo mjini pekee.
Amidulah Amesema na kwa vile wao ni wadau wa vibanda walishalipa
lakini kukarabati  kwa machinjio hiyo imekuwa ni kizungumkuti
aliendelea kusema kuwa  halmashauri inakusanya fedha nyingi kupitia
mifugo kwani wao hulipa ushuru mnadani kila kichwa cha ng’ombe wao
hulipa shilingi sita na ng’ombe akifika machinjioni wao hulipa ushuru
wa chinjio shilingi elfu tatu kwa kila kichwa cha ng’ombe anayechinjwa
hivyo wao kama wao hali ya kusema halmashauri haina fedha haiwaingii
hakilini .
Mwenyekiti huo amesema anamtaka mkurugenzi wa halamashauri hiyo asema
ukweli kuwa hawataki kukarabati wala kufanya usafi hivyo waache
wanannchi wafe.lakini amesema kuwa TFDA pamoja na kuchukia hatua hiyo
ya kufunga machinjio wao wamewapongeza lakini imewagharimu wao kwa
kuwa hiyo ndiyo ajira yao ambayo wanapatia mkate wao wa kila siku pia
wanasomesha watoto kwa kuuza nyama lakini haitoshi wanannchi wa wilaya
ya Bukombe wamekosa nyama ambayo ni kitoweo walichozoea ambacho kina
gharama nafuu kuliko kuku na samaki. Hivyo mkurugenzi James Ihunyo na
idara yake wamesababisha hayo wanawaomba na kuwataka wahakikishe
wanakarabati vinginevyo wataandamana hadi ofisini kwake kudai huduma
ya nyama wakiambatana wafanyabishara wa nyama na wananchi ndani ya
siku mbili.
MWISHO

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply