sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » KIKUNDI CHA WAFUGAJI CHAFUNGUA FURSA YA MASOKO KWA WAFANYABIASHARA.

Kikundi cha wafugaji kata ya Ulowa katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kimetoa wito kwa wafanyabiashara wa mifugo na mazao katika wilaya ya Kahama na wilaya jirani kujitokeza kufanya biashara katika soko la Ulowa liliofunguliwa hivi karibuni.
 
Wito huo umetolewa jana na mwenyekiti wa Kikundi hicho Magida Pambe wakati akiongea na  kuhusu uanzishwaji wa soko hilo litakalohusika na uuzaji wa Mifugo na mazao katika halmashauri hiyo.
 
Pambe amesema kuwa soko hilo linalopatikana katika kijiji cha Kangeme litajumuisha biashara ya mifugo ikiwemo Ng’ombe,Mbuzi,Kondoo na kuku pamoja na mazao ya nafaka yakiwemo Mpunga,Mahindi,Maharage na Karanga.
 
Pambe ameongeza kuwa soko hilo linalofanyika siku ya jumapili lina eneo kubwa la kuegesha magari na kwamba miundo mbinu katika soko hilo ni mizuri ikiwemo barabara inayofikika kirahisi hadi katika eneo la soko.
 
Katika hatua nyingine katibu wa kikundi hicho ambaye pia ni Afisa Kilimo na Mifugo kata ya Ulowa Charles Malimi amewahakikishia wafanyabiashara kusimamia ukaguzi na matibabu ya mifugo ikiwa ni pamoja na ubora wa mazao yanayouzwa katika soko hilo.
 
MWISHO

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply