sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » Lowassa Morogoro

MWANASIASA Mkongwe wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Juma Ngasongwa, amesema chama hicho kimeyumba kiongozi kinamuhitaji, Edward Lowassa kukirudisha katika mstari.
Dk. Ngasongwa aliyasema hayo katika mkutano wa kumkabidhi orodha ya wanachama waliojitokeza kumdhamini Lowassa katika mbio zake za urais kwenye Ofisi za CCM, Mkoa wa Morogoro.
Katika mkoa huo Lowassa alipata wadhamini 100,438 kutoka katika Wilaya za Kilosa (8,300), Morogoro Vijijini, (6,680), Muvumero(11,870), Gairo (1,850), Ulanga (13,000), Kilombero () Morogoro Mijini  (27,100)Mkoa wa Morogoro ni mkoa wa 31 na mwisho kati ya aliyotembelea Lowassa na kupata jumla ya wadhamini 863,479.Dk Ngasongwa alisema viongozi wa CCM katika kipindi cha katikati waliyumba baada ya kufanya kazi za kukiinua chama wameingia kwenye malumbano.
"Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi hapa katikati wanayumba wapo waliowaambia wenzao ni mwaziri mzigo wengine ni wagombea wanatukana wenzao hakuna wa kuwakemea hajulikani ni nani msemaji wa chama.
"Sasa nasema anayetakiwa kukirudisha chama katika mstari ni mwanaCCM imara naye ni Edward Lowassa,"alisema Dk. Ngasongwa.
Naye mwanasiasa Mkongwe, kanali mstaafu Isack Mwisongo alisema kumekuwa na maneno mengi kutoka kwa baadhi ya wanachama wa chama hicho kuwa Lowassa alikataliwa na Mwalimu Julius Nyerere hayana ukweli.
"Sielewi nianzie wapi na niishie wapi niakufahamu tangu mwaka 1976 ulipojiunga katika chama chetu ukiwa kijana mdogo wewe pamoja na wenzako akina Ditopile Mzuzuri(marehemu) Jakaya.
"Nikakufahamu zaidi wakati nafundisha chuo cha uongozi pale Monduli na Mkuu wa Utawala wa chuo baadaye nikaingia katika vikao vya maamuzi vya chama.
Sikuwahi kusikia Mwalimu akikukataa nimekuwa mjumbe wa NEC sikuwahi kukosa hata kikao hata kimoja sikuwahi kusikia hivyo wanakuzushia tu, Nyerere hakuwa mnafiki akikukataa anakufukuza na anatangaza katika televisheni ya TBC kuwa amekufukuza," alisema Kanali Mwisongo.
Alisema Lowassa ni mtu anayewapenda Watanzania siku zote za maisha yake.
Alisema kuna wakati alitokea mwekezaji mmoja ambaye alijua chanzo cha gesi cha Msimabati, akataka eneo hilo kwa kujifanya anajenga hoteli ambayo itakuwa na vyumba kumi Lowassa alikataa.
Alisema kuwa Lowassa amabye wakati huo alikuwa Waziri wa Ardhi na Nyumba alikataa kwa kuwa alikuwa anajua janja ya huyo mwekezaji kwani shida yake haikuwa kujenga hoteli bali gesi.
"Kwa watani zangu wa Mtwara nataka niwaambie bila Lowassa hiyo gesi wasingeipata kwani kuna mkubwa mmoja alimpa mgeni mmoja ajenge hoteli katika chanzo cha gesi lakini baada ya kufika kwa Lowassa, Lowassa aligoma.
"Lakini mkubwa yule alimuita mkubwa wa kati na Lowassa akamwambia huyu bwana mdogo anajeuri nimemleta mtu aweke hoteli msimbati lakini amekataa yule Bwana mkubwa akamuuliza Lowassa wewe unasemaje, Lowassa alijibu kuwa huyu mtu anataka chanzo cha gesi si kujenga hotel bali ni gesi," alisema Kanali Mwisongo.
Alisema uamuzo huo wa Lowassa ukasababisha huyo mgeni kukosa hilo eneo ambalo angepewa kwa miaka 99.
Kanali Mwisongo alimunukuu mwalimu Nyerere kuwa ni bora kiongozi anayetoa anayekosea kwa kutoa maamuzi yenye manufaa kwa watanzania lakini CCM sasa imekuwa na maamuzi yasiyo na manufaa kwa wananchi.
Alisema viongozi wa chama hicho maamuzi kabla ya vikao vilivyokaa wanaharibu chama hicho.
Alisema chama kinayumba wanachama wamevumilia na wamewataka viongozi hao kuacha kukiyumbisha chama hicho.
"Tunaomba CCM wasifanya makosa tunajua katika kamati kuu kutakuwa na mizengwe, kamati na ya maadili kutakuwa na mizengwe lakini halmshauri kuu inauwezo wa kurudisha jina lolote hata kama liko katika kapu," alisema Kanali Mwisongo.
Waziri Mkuu mstaafu, Lowassa alisema akipata madaraka hayo atahakikisha  anairudisha Morogoro kuwa mji wa Viwanda kama zamani ili kuongeza soko la ajira kwa vijana.
Alisema Rais Jakaya Kikwete amefanya kazi kubwa na nzuri sasa anaondoka na kumuachia kijiti mtu mwingine naye ni yeye (Lowassa).
Alisema kwa kuwa mkoa huo, uliahidiwa  kuwa na ghala kubwa la chakula na haikuwa hivyo,akifanikiwa kuingia madarakani jambo kwanza ni kuhakikisha analifanyikazi suala hilo.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply