sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » MWANDISHI WA HABARI AJITOSA UBUNGE KAHAMA

 MWANDISHI WA HABARI WILLIAMU BUNDALA AKIHUTUBIA MAELFU YA WAFASI WA CHADEMA KATIKA KATA YA USHETU WILAYANI KAHAMA AMBAPO TUME YA UCHANGUZI IMETANGAZA USHETU NI JIMBO LA UCHANGUZI MWAKA HUU AMBAPO TUMIE IMETANGAZA MAJIMBO 26 MAPYA.
 BAADHI YA WANACHNGAZA WA CHADEMA WAKIMBA JUU MGOMBEA WAO WA CHADEMA WILLIAMU BUNDALA BAADA YA KUTANGAZA AZIMA YAKE. 
BAADHI YA WANANCHI WA KATA YA USHETU WAKISIKILIZA HOTUBA YA MUWEKA AZIMA Na  

Kahama

MWANDISHI WA HABARI HAJITOSA UBUNGE KAHAMA

MWANDISHI wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi k” ameamua  kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Ubunge katika Jimbo la jipya la Ushetu katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu mkoani Shinyaga,kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA.

Bundala ametangaza kuingia kwenye mchakato wa kugombea kuteuliwa na Chama ili aweze kupeperusha bendara katika uchaguzi mkuu ujao katika mkutano wake wa kutangaza nia uliofanyika katika Kijiji cha Bogomba “B” kata ya Ubagwe wilayani Kahama.

Mtia nia huyo alisema endapo Chama chake kitampitisha na hatimaye kushinda Ubunge katika Jimbo hilo atahakikisha anasukuma kasi ya maendeleo katika jimbo hilo jipya lenye Rasimali nyingi kupitia nafasi yake na wajibu kama anavyotakiwa Mbunge Kufanya.

Alisema kuwa dhamira yake imemsuta kwenda kuwatumikia wananchi wa wilaya hiyo ambayo yeye ni mzawa na kuwa atahakikisha anapigania
maendeleo ya wananchi kwa kasi huku akiondoa uonevu kwa waandishi wa
 habari na watumishi wengine serikalini na katika halmashauri za
wilaya.

Sambamba na hayo amesema kuwa sababu nyingine iliyomsukuma ni kuona wagombea wengine wanaolitaka jimbo hilo hawako kwa ajili ya ukombozi wa jimbo hilo bali wako kwa ajili ya maslahi binafsi  kutokana na asilimia kubwa ya wagombea hao si wakazi wa eneo hilo na kwamba hawafahamu matatizo ya wana ushetu kama anavyoyafahamu yeye.

Aliongeza kuwa akifaniiwa kuukwaa Ubunge pia atasimamia kuhakikisha Jimbo hilo jipya linapata Chuo cha ufundi kwa ajili ya vijana wanaomaliza darasa la saba na kidato cha nne kupata elimu jambo lilatalopunguza wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana.




Bundala alisema kipaumbele kingine atakachoshughulikia ni pamoja na kusimamia na kutoa elimu ya Sheria kupitia wanasheria ambao watazunguka katika kata kutoa elimu hiyo hususan katika maswala ya umiliki wa Ardhi,Mirathi,haki za wakulima na wafugaji pamoja na haki za raia na mali zao kwa ujumla.

Akizungumzia kuhusu suala la michezo katika jimbo hili Bundala amesema kuwa kupitia Kijukuu Cup atahakikisha anashirikiana na halmashauri na wadau wa michezo kuhakikisha halmashauri ya ushetu inapata timu ya kucheza ligi kuu Tanzania Bara.

Awali Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CHADEMA (BAVICHA) Halmashauri ya Ushetu Emmanuel Magema aliwataka vijana wote kuungana ili kumuunga mkono kijana mwenzao aliyejitokeza na kuonesha nia ya kutaka kuongoza akiwa Mbunge wa jimbo hilo.

Wilaya ya Kahama kwa sasa ina halmashauri za wilaya tatu za
 
Msalala,halmashauri ya mji wa Kahama na halmashauri mpya ya Ushetu na kufanya majimbo ya uchaguzi kuwa matatu.

Katika kinyang’anyiro cha Ubunge katika jimbo jipya la Ushetu kuna watu zaidi ya watano wanaotajwa kulimendea jimbo huku wagombea wa CHADEMA wakionekana kuungwa mkono na makundi mengi hususan vijana

MWISHO 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply