Watu watano wamefariki na wengine sita kujeruhiwa katika ajali ya gari
iliyokea kijiji cha Matandalani wilaya ya Mlele mkoani Katavi baada ya
gari aina ya NOAH lenye namba T 451 DDP ikitokea Mpanda mjini Kuelekea
Sitalike kupinduka na kuacha njia.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari amesema ajali hiyo
imetokea majira ya saa tano za asubuhi baada ya gari kupasuka tairi na
kupinduka ambapo chanzo cha ajali kikiwa mwendo kasi.
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Mpanda Daktari Teopista
Elista anasema walipokea majeruhi na miili ya marehemu majira ya saa
sita mchana na kudai kuwa miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika
hospital hiyo.
Majeruhi wa ajali hiyo wanaendelea na matatibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Watoto wenye miezi tisa na miaka mitatu wamenusurika uku mama yao akipoteza maisha
Dereva wa gari hilo aliyejulikana kwa jina la Jastini Sizyindayasa anashikiliwa na polisi.
Katika hatua nyingine miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika chumba
cha maiti hospitali ya Mpanda uku vifaa vya kuhifadhia Maiti vikiwa
vimeharibika.
Chanzo-Eddy Blog
No comments: