ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA SHINYANGA KHAMIS MGEJA AKIWASILI KATIKA UWANJA WA MITUMBA SHINYANGA KATIKA MOJA YA KAMPENI ZA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA
Anayehitaji mabadiliko
hatokuwa tayari kuona Wakala anapindisha dhamira yake lazima atatetea haki yake
kwa namna yoyote ile hivyo isifikie vikatokea vitendo vya uvunjifu wa amani
mara baada ya matokeo kutangazwa.
Mgeja amesema kuwa Mawakala wanaoteuliwa na chama kwenda
kusimamia zoezi la kupiga na kuhesabu kura wanabeba mamilioni ya Watanzania
wenye Mapenzi mema na Taifa hivyo kukubali kwao kununuliwa na CCM ni wazi
watakuwa wamesaliti kundi kubwa linalohitaji Maendeleo.
MH KHAMIS MGEJA AKIHUTUBIA WAKAZI WA JIMBO LA SHINYANGA MJINI
Mbunge kwa
tiketi ya CHADEMA Patrobus Katambi jimbo la Shinyanga Mjini Alishikwa Mkono na Mgeja kuomba kura
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoani
Shinyanga kimewaonya vikali Mawakala wa
Uchaguzi wa Chama hicho katika uchaguzi mkuu juu ya kuhujumu chama, kwani
kuteuliwa kwao na chama wamebeba dhamana ya Watanzania wengi wanaotaka
Mabadiliko.
Kauli hiyo ilisemwa na aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha
Mapinduzi mkoa wa Shinyanga ambaye ni mjumbe wa timu ya Kampeni ya UKAWA Taifa
Hamis Mgeja alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mkoa huo katika Mikutano ya
kampeni ya chama hicho.
No comments: