Baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi
Zanzibar, ZEC kutangaza kufuta matokeo ya Uchaguzi mkuu wa Zanzibar
October 28 2015, Kiongozi wa zamani wa chama cha CUF, Professor Ibrahim
Haruna Lipumba na mgombea Urais wa Zanzibar kwa mwamvuli wa CUF na Umoja
wa vyama vya UKAWA, Maalim Seif Sharif Hamad wamezungumzia kuhusu
kuchukuliwa kwa hatua hiyo.
“Nimeshtushwa na hatua hiyo hasa
ukizingatia Uchaguzi umefanyika tarehe 25 leo ni tarehe 28, na sababu
ambazo Mwenyekiti amezitoa ni mambo ambayo yangeweza kujulikana mapema
sana… Tume ya Uchaguzi ya Taifa ambayo inatangaza matokeo ua Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa inatangaza Kura za matokeo ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano ambazo zimefanyika kwenye uchaguzi huohuo
mmoja na Tume haijasema kwamba uchaguzi ule ulikuwa mbovu.”- Professor
Ibrahim Haruna Lipumba.
“Hata watazamaji wa Kimataifa wamesema
utaratibu wa kupiga Kura na kuhesabu vituoni ulikwenda vizuri… nashukuru
viongozi wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amewaomba Wazanzibar kuwa
watulivu wakati suala hili linashughulikiwa.” >>> Prof.
Lipumba.
“Ilipaswa iundwe Tume ya Majaji watazame
tamko alilolitoa lina uhalali gani, wazungumze pia na Wajumbe wa Tume
ya uchaguzi kwa sababu tamko hilo limevunja Sheria halina uhalali wa
kisheria.”
Hili ndio jibu la Professor Lipumba kuhusu anayeweza kumaliza tatizo lililotokea Zanzibar >>> “Mtu ambaye ana uwezo na wajibu mkubwa kwenye hili ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa sababu yeye ni Rais na Mwenyekiti wa CCM, ashauriane na Rais wa Zanzibar ili akubali kuunda Serikali ya kitaifa, imefika wakati Dk. Shein aoneshe ukomavu wa kisiasa.”
“Kuna watu wamelalamika, nimemsikia
Edward Lowassa amelalamikia matokeo ya Uchaguzi, haya ambayo Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ameyaeleza yanaongeza nguvu kwa Mheshimiwa
Lowassa kwamba hata Tanzania bara mambo hayakwenda sawa… Hatua
aliyochukua Mwenyekiti imevunja Sheria, isipotokea ufumbuzi mapema,
patatokea vurugu.” >>> Professor Ibrahim Haruna Lipumba.
HAPA NAANZA NA KILE ALICHOKISEMA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD.
“Chama cha CUF kimepata taarifa kwamba
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar ametangaza kufuta matokeo ya
uchaguzi mkuu bila kuwashirikisha Makamishna wenzake wa Tume ya
Uchaguzi…. CUF imeshtushwa na taarifa hii ambayo iko kuinyume na Sheria
za uchaguzi ya Zanzibar, Mwenyekiti hana mamlaka ya kufuta Uchaguzi
huo.” >>> Maalim Seif Sharif Hamad.
“Mwenyekiti hakutafakari kwamba kuufuta
uchaguzi Zanzibar kunaathiri pia Uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa sababu wapiga Kura ni walewale waliomo kwenye daftari la
wapiga Kura wa ZEC.” >>
“Rais wa Jamhuri ya Muungano hawezi kupatikana kwa kupigiwa Kura na wananchi wa Tanzania bara pekeyake… Tunatambua kwamba hatua hii imekuja baada ya majaribio ya kulazimisha ushindi kushindikana.”
“CUF hatutambui uamuzi huo wa Mwenyekiti
wa Tume ya ZEC, tunaitaka Serikali na CCM kuiacha Tume iendelee na
uhakiki wa matokeo na itangaze mshindi… Tunatoa wito na kuomba
Wazanzibar kwa ujumla kubaki watulivu..” >>> Seif Sharif Hamad.
Sauti yote ya Maalim Seif Sharif Hamad hii hapa kama umepitwa na hii taarifa,pia kuna sauti ya Professor Ibrahim Lipumba
Sauti yote ya Maalim Seif Sharif Hamad hii hapa kama umepitwa na hii taarifa,pia kuna sauti ya Professor Ibrahim Lipumba
No comments: