Msimamizi wa Tume ya uchaguzi Halmashauri ya msalala Mwenye kofia Patrick karangwa Akiangalia jinsi matokeo ya Ubunge yanavyoingizwa katika mfumo wa Mtandao kabla ya kutangaza Matokeo .
Wasimamizi wa Uchaguzi jimbo la Msalala wakiwa katika kuhakiki Matokeo ya Wapiga kura jimbo la Msalala
Wasimamizi wa Tume ya uchaguzi wa Tunajumlisha Kura za jimbo la Msalala
Tunaendelea Kupokea Matokeo
Tunakusanya Matokeo jimbo la Msalala
Mwanasheri wa Halmashauri ya Msalala Wakihakiki Matokeo ya kura Jimbo La Msalala
Wasimamizi wakijaribu kuweka Mambo sawa ya matokeo ya Kura
Wasimamizi wa Tume wakifanya Majumuisho ya Matokeo ya kura za jimbo la Msalala
Mgombea wa jimbo la Msalala kupitia CCm Ezeikiel Maige Mwenye Tshet ya Mistali huku akiwaonyesha kidole Mwaandishi wa Mwanachi juu ya Kusubiri matokeo katika Viwanja Vya Halmashauri ya msalala
Waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari wakiwa katika Ukumbi wa Halmashauri ya Msalala wakisubiri Matokeo.
Tusubirini Tu matokeo
Ilipofika majira ya saa 12 jioni Msimamizi wa Tume Ya Uchaguzi Patrick Kurangwa Alitangaza matokeo kwa Waandishi wa Habari
Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la msalala Patrick Kurangwa alifafanua baadhi ya kasoro zilizijitokeza katika zoezi la upingaji wa kura .
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Msalala Akiwa ofisi kwake Akieleza waanahabari hali ya Zoezi zima la Uchaguzi ilivyoendehwa kwa Utulivu na Amani
Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Ushetu Isabela Chilumba akionea na Waandishi wa Habari juu ya kuchelewa kutolewa Kwa matokeo ya Uchaguzi Jimbo la Ushetu .
KAHAMA
Tume
ya uchaguzi imemtangaza Kwandikwa Elias kuwa mbunge wa jimbo jipya la
Ushetu akiwashinda wagombea wengine ambao ni Lubala Dotto wa ACT,Kitibu John wa
NCCR Mageuzi na Isaya Bukakiye kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA.
Akitangaza
matokeo ya uchaguzi huo Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo Isabela
Chilumba alisema Kwandikwa aliyekuwa akigombea kupitia chama cha Mapinduzi CCM
ameshinda kwa kura 50365 sawa na asilimia 65.44 kati ya kura halali zilizopigwa
73101.
Wakati
huohuo tume ya uchaguzi ilimtangaza Ezekiel Maige kupitia chama cha Mapinduzi
kuwa Mbunge wa jimbo la Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga akiwashinda
wagombea wengine Paul Malaika wa CHADEMA,Abeid Iheshi wa UPDP na Michael Sua wa
ACT.
Maige
alitangazwa kuwa mbunge na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo Patrick Karangwa
kwa ushindi wa kura 36010 kati ya kura halali 57059 zilizopigwa huku Malaika
Paul wa CHADEMA akipata kura 20124,Michael Sua wa ACT kura 674 na Abeid Iheshi
akipata kura 251.
No comments: