Emmanuel Nzungu, mmoja wa timu ya kampeni ya mgombea urais kupitia ukawa, Edward Lowassa akinadi sera za CHADEMA kwa umahili katika mkutano wa kufunga kampeni mjini Shinyanga
Nzungu akimwombea kura, Mgombea urais kupitia UKAWA, Edward lowasa, Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga, Patrobas Katambi na madiwani wa kata zote za manispaa ya Shinyanga.
Akahitimisha kwa kuwataka wanashinyanga kufanya mabadiliko ya uongozi wa nchi hapo kesho.
Umati mkubwa wa watu wenye matumaini na viongozi wanaotokana na UKAWA, mjini Shinyanga
Nguli wa siasa, Khamis Mgeja, akiwahutubia wananchi wa manispaa ya Shinyanga waliojitokeza kwa wingi katika mkutano wa kuhitimisha kampeni uliofanyika katika viwanja vya Shycom, mjini Shinyanga
Ilikuwa ni mafuriko ya CHADEMA katika mkutano wa kufunga kampeni manispaa ya Shinyanga katika viwanja vya shycom
Wapenzi wa mabadiliko wenye imani na uongozi watakaoupigia kura hapo kesho katika manispaa ya Shinyanga viwanja vya shycom
Wanashinyanga wakipunga mikono juu kwa shangwe wakishangilia mabadiliko wakati viongozi wa kamati ya kampeni za uchaguzi timu ya Edward Lowasa wakiongozwa na Khamis Mgeja.
Hapa ni Shingwe tu za wana Ukawa na mabadiliko katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga
Patrobasi Katambi, Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini akiwahutubia wananchi wa manispaa hiyo akiomba ridhaa ya kushika kiti cha ubunge ili awaletee maendeleo ya kweli na mabadiliko ya kweli.
Katambi alitumia mkutano huo wa kuhitimisha kampeni kutangaza vipaumbele vyake iwapo atapata ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo la shinyanga kwa atashughulikia sekta za maji, afya, umeme, miundombinu, kilimo na mifugo.
No comments: