Maeneo ya machimbo ya nyangalata wilayani kahama ambapo zaidi ya watu saba wamepoteza maisha yao na wengine kujeruhiwa vimbaya mili yao
Moja ya shimo ambalo liliotitia likiwa na watu zaidi ya kumi na baadhi yao kupoteza maisha katika majimbo madogo ya nyangalata.
Haya ni baadhi ya mashimo ambayo wachimbaji wandogo hufanyakazi za kuchimbaji wa madini hayo ya dhahabu
Baadhi ya wachimbaji katika eneo la nyangalata wakiwa katika huzuni kubwa baada ya jamaa zao kupoteza maisha na wengi wakiwa bado wanaendelea kuopolewa.
Eneo ambalo limepoteza maisha ya wachimbaji wadogo takribani saba na wengi wako mahututi na huku baadhi ya ndugu zao wakiangali eneo la watu hao walifukiwa na kifusi hicho
Hii ndiyo mifuko yenye mawe ya dhahabu ambayo wachimbaji wadogo hutoka nayo zaidi ya fut mia
Baadhi ya eneo la machimbo ambapo wachimbaji wadogo wamepoteza maisha yao na wengi kupata majeraha makubwa katika mili yao
Moja wa wachimbaji wadogo akiopolewa na wachimbaji wenzeka baada ya kunusurika kifo katika machimbo ya nyangalata wilayani kahama
Baadhi ya wachimbaji walikwisha opolewa toka chini ya mashimo hayo ya dhahabu huku wangine wakipoteza maisha yao.
Watu 7 wanadaiwa kufariki Dunia kwa kufukiwa na kifusi cha udongo katika machimbo
ya dhahabu yaliyopo katika kijiji cha
Nyangarata kata ya Lunguya wilayani
Kahama mkoani Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja waliofukiwa kuwa ni Chacha
Wambura(54) mwenyeji wa Bunda mkoani Mara,Msafiri Gerald(30) mwenyeji wa
Sumbawanga.
Wengine ni Onyiwa Kaindo(55) mwenyeji wa Tarime,Mussa Supana
(29)mwenyeji wa Magu mkoani Mwanza,Amos Mwangwa(20) mwenyeji wa Misungwi mkoani
Mwanza,Joseph Bulule(35) mwenyeji wa Mugumu Serengeti pamoja na Dani
Makwesa(30) mwenyeji wa Ngasamo Nyashimo.
Kamugisha alisema kuwa tukio hilo limetokea tarehe 6 Oktoba
mwaka huu majira ya saa 5 asubuhi wakati wachimbaji wadogo wakiendelea na
shughuli za uchimbaji ndipo eneo la juu la Machimbo hayo lilipotitia na kuwafunika wachimbaji hao.
No comments: