Alikuwa mbunge wa jimbo la kahama Jemes Lembeli kwenye Moja ya mikutano ya kampeni Mjini kahama
Lembeli ameiambia Dunia Kiganjani Blog leo kwamba taarifa
zote zinazotolewa kupitia akaunti hiyo yenye jina la "James Lembeli"
na picha yake akiwa na aliyekuwa mgombea urais wa Chadema kupitia mwavuli wa
UKAWA Edward Lowassa ni za uongo.
Amewataka watu wanaoguswa na taarifa hizo kuzipuuza, huku
akiwaonya waliofungua akaunti hiyo waache mara moja na kwamba akiwabaini
atawashitaki kwa mujibu wa sheria.
Lembeli ameliomba jeshi la polisi kupitia kitengo cha
Intelligensia kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ya makosa ya mitandao kumsaka
mtu aliyefungua akaunti hiyo na kumtia nguvuni.
No comments: