Mama Regina Lowassa.
Mke wa aliyekuwa Mgombea Urais kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mama Regina Lowassa.
Mama Regina Lowassa Akiwa katika moja ya Mikutano ya kampeni Mkoa wa kilimanjaro jimbo la hai
DAR
Ameikataa kwa nia njema nafasi aliyopewa ya kuwa mbunge wa
viti maalum kupitia chama hicho.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ilitangaza mgawanyo wa viti
maalum jana ulioonyesha kuwa Chadema imevuna viti 36, ikiwa ni ongezeko kubwa
lililotokana na kufanya vizuri zaidi katika majimbo kulinganisha na uchaguzi wa
mwaka 2010 wakati walipopata idadi ya viti maalum isiyokaribia 30.
Taarifa iliyopatikana jijini Dar es Salaam jana ilieleza kuwa
mama Lowassa ambaye alifanya kazi kubwa ya kupigania mafanikio ya Chadema
wakati wa kampeni, ameikataa kwa nia njema nafasi hiyo aliyopewa na kamati Kuu
ya Chadema.
Ilielezwa kuwa Mama Regina aliipokea kwa heshima nafasi hiyo,
lakini anaamini bado anao uwezo wa kushughulikia matatizo ya akina mama na
watoto akiwa nje ya bunge.
"Naishukuru kamati kuu ya chama changu kwa heshima hii
kubwa waliyonipa na ninaithamini sana. Lakini naamini nitaendeleza mapambano ya
kuwaletea kina mama mabadiliko na kwa ufanisi zaidi nikiwa nje ya bunge,"
Mama Lowassa alikaririwa akisema.
Kamati Kuu ya Chadema iliamua kumtunuku nafasi ya ubunge viti
maalum kutokana na mchango mkubwa alioutoa wakati wa kampeni ambao kwa kiasi
kikubwa ulisaidia upatikanaji wa kura nyingi kwenye majimbo ya uchaguzi na
mwishowe chama hicho kikatangaziwa na NEC kupata nafasi 36 za viti maalum.
No comments: