sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » CHADEMA WAIOMBA SERIKALI MABATI WALIOPA WAHANGA WA MWAKATA



























KAHAMA 

Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA wilayani Kahama Mkoani Shinyanga Kimetoa tamko la Kuiomba Serikali kurejesha Msaada wa mabati zaidi ya 800 yaliyotolewa na Chama hicho kwaajili ya ujenzi wa Nyumba za wahanga wa Mafuriko

Tamko la Chama hicho kudai msaada huo limetolewa na Mwenyekiti wa Chama hicho Juma Protase Ntaimpera ambaye alisema  azimio la Chama hicho linatokana na Tamko la Rais John Magufuli kubainisha kuwa Serikali haina nia ya kujenga nyumba za wahanga hao

Ntaimpera alisema  kutokana na tamko hilo la Rais alilotoa wakati wa ziara yake Wilayani Kahama mwshoni mwa mwezi julai mwaka huu,CHADEMA waliandika  barua kwa Mkuu wa Wilaya kuitaka Serikali kurejesha msaada huo

Mwenyekiti huyo,alisema baada ya serikali kurejesha Mabati hayo Chama kitayagawa kwa watu wenye mahitaji ili wayatumie katika ujenzi kwakuwa wanaishi katika mazingira magumu.   

Ntahimpera aliongeza kuwa ,CHADEMA walitoa msaada huo kwa nia njema kwaajili ya kuwasaidia wahanga wasiojiweza hasa kwakuzingatia umu wa maisha wanaokutana nao baada ya Mvua kubwa iliyoambatana na Upepo mkali kuezua nyumba zao ,baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mwakata  kata ya Mwenda ulimakubaki bila makazi na wengine kupoteza maisha

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply