ENEO LA MAZIKO MHONGOLO LAPATIWA UFUMBUZI KAHAMA

Mwenyekiti wa Halmashauri mji wa kahama Abel shija 

KUFUATIA mgogoro baina ya wananchi na ofisi ya kata ya Mhongolo wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga, kuhusu eneo lililokuwa klimetengwa kwaajili ya huduma za kijamii na kuvamiwa na baadhi ya wananchi waliojenga makazi ya kuishi halmashauri ya mji huo imelipatia ufumbuzi.

Hali ya kupatikana kwa eneo hilo imekuja baada ya siku chache wananchi wa mtaa Mhongolo kwenda na jeneza katika ofisi ya afisa mtendaji wa kata Maziku hiyo Mbusili na kulazimisha wazike mbele ya ofisi yake kwa madai wamekosa eneo la kuzika kutokana na eneo lao liliuzwa na diwani Michael Mizubo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama, Abel Shija aliyeongozana na wataalamu wa ardhi kutoka halmashauri huku wakiwa wamebeba lamani nzima ya kata hiyo walifika katika eneo la bega kwa bega naa kuonesha mipaka ya eneo hilo la maziko na kuwakabidhi wahusika ili waendelee kupata huduma hiyo muhimu.

Aidha mwenyekiti huyo wa halmashauri wakati akiwaonyesha mipaka wananchi hao aliwataka waanze mara moja kupata huduma hiyo huku akidai kuwa pamoja na ramani hiyo kubainika kuwa na mapungufu haiwazuii kupata huduma hiyo na kuwaagiza wataalamu hao wa ardhi kufanya maboresho ya ramani hiyo kwa kuongeza eneo la soko na uwanja wa mpira.

MWISHO 


ENEO LA MAZIKO MHONGOLO LAPATIWA UFUMBUZI KAHAMA ENEO LA MAZIKO MHONGOLO LAPATIWA UFUMBUZI KAHAMA Reviewed by Mohab Dominic on 06:18 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.