Mkurungezi wa Mji wa kahama Anderson Msumba |
MKURUGENZI mtendaji wa halmashauri ya mji wa Kahama mkoa wa Shinyanga
Anderson Msumba amemuondoa kwenye nafasi yake ya kazi mhasibu wa hospitali ya
mji huo, Mirian Mwakasenge kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha.
Mwakasenge pia anatuhumiwa kuihujumu hospitali hiyo kwa
kuingiza dawa zake hospitalini humo na kasha kuwauzia wagonjwa dawa zake
binafsi badala ya dawa za hospitalini.
Hatua hiyo ya Msumba ni utekelezaji wa agizo la mkuu wa
wilaya hiyo Fadhil Nkurlu ambaye hivi karibuni aliuagiza uongozi wa hospiali hiyo
kuwawajibisha watu wote waliohusika kufuja fedha za mapato ya hospitalini na
kusababisha kupungua kwa mapato kutoka sh. milioni 45-20 kwa mwezi.
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana Msumba alisema
kuwa kutokana na agizo hilo la DC, uongozi wake ulifanya uchunguzi wa kina na
kubaini chanzo ni mhasibu wa hospitali hiyo kuingiza dawa zake hospitalini na kuwauzia
wagonjwa dawa zake binafsi.
“Hospitali ya mji inahudumia wagonjwa wengi sana
na asilimia kubwa inahudumia wagonjwa wa halmashauri tatu za Ushetu, Msalala na
Kahama mji pamoja na wilaya jirani za
Bukombe, Mbogwe, Nyang’hwale na Nzega lazima mapato yangekuwa juu lakini kwa
sasa mapato yapo chini, hii inatokana na ubadhilifu unaazia kwenye uandikishaji
wav yeti dirisha la malipo na inaonyesha Tehama inachengeshwa ili kufanyika kwa
wizi,” alisema Msumba
No comments: