LICHA ya halmashauri ya
mji wa Kahama mkoani Shinyanga kukiri kukabidhiwa majengo yaliyokuwa yakitumiwa na hamlamashauri ya Ushetu kama ofisi wakati wakiendelea na ujenzi wa makao makuu huko Nyamilangano lakini majengo hayo yamekabidhiwa
rasmi yakiwa yamechakaa huku madirisha ya vioo yakiwa yamevunjwa na watumishi wake hali ambayo nyaraka za ofisi zimezagaa na kuoneka holela.
Hali hiyo ilielezwa na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama, Abel Shija wakati akizungumza na
wandishi wa habari muda mfupi baada ya kamati ya fedha na uchumi kufanya ziara
ya kukagua miundo mbinu ya majengo waliyokabidhiwa na kujionea uharibifu uliofanywa na watumishi wa halmashauri hiyo baada ya kugundua wanaondoka huku wakitakiwa kuziacha nyaraka zao.
Shija amewambia wandishi
wa habari kuwa kulingana na majengo hayo yaliyokabidhiwa na halmashauri ya
Ushetu kwa mji ukarabati wake wake unahitaji kiasi kikubwa cha fedha
hali ambayo halmashauri itaingia hasara kubwa katika ukarabati wa miundo mbinu wa majengo hayo.
“Kwa usahihi wa jambo
hili kwanza tuishukuru sana serikali kupitia Tamisemi ka sababu imeliona jambo
hili lakini pia imewezesha tufante usafi na ukarabati mapema wa majengo haya
yaliyokuwa yametelekezwa pamoja na kurejesha majengo haya
yaliyokuwa hapo awali yakitumika kama majengo ya halmashauri ya wilaya ya
Kahama na baadaye baada ya kupatikana kwa halmashauri tatu za Ushetu, Msalala
na Mji yenyewe, licha ya kukabidhiwa majengo haya wameyaharibu sana kwa
kuyachakaza,” amesema Shija mwenyekiti wa halmashauri ya mji.
Pia mwenyekiti huyo
amesema kuwa baada ya watumishi wa halmashauri kupata taarifa ya kuondoka
katika majengo hayo na kurudi katika makao makuu ya halmashauri yao yaliyoko katika Kata ya Nyamilangano badala ya kukabidhi majengo yakiwa na hali nzuri badala yake waliamua kupasua vioo vya
madirisha huku nyaraka mbalimbali za ofisi zikionekana jambo ambalo ni hatari.
Kwa upande wake
mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kahama Anderson Msumba alisema kuanzia 2014 majengo
hayo yalikuwa yamekabidhiwa kwa halmashauri ya mji lakini Ushetu waliomba wakae
kwa muda wakati ujenzi wa makao makuu huko Kata ya Nyamilangano unaendelea.
Hata hivyo kwa taarifa za kuaminika kutoka chanzo chetu cha habari wilayani hapa kimesema kuwa kufuatia halmashauri makabidhiano hayo ya makao makuu ya ofisi mjini Kahama baadhi ya Madiwani wa halmashauri ya Ushetu wamepanga kumgawana mkurugenzi mtendaji Michael Matomola na kutishia kumfungia ndani kutokana na amekabidhi majengo hayo bila kushirikisha baraza la Madiwani hao.
|
No comments: