|
Baadhi ya wakazi wa kata ya mhongholo wakiwa wamebeba saduku la mtoto mchanga kuja kuzika katika ofisi ya mtendaji |
|
JENEZA LA MTOTO LIKIWA NJE YA OFISI YA MTENDAJI KWA AJILI YA MAZIKO |
|
Diwani wa kata ya mhongholo mh michael Mizubo akiwaomba wananchi kuwacha kufanya kitendo hicho |
|
hili ndiyo kaburi lilochimbwa katika ofisi ya mtendaji kwa tuhuma ya kuuza maeneo ya maziko yenye na diwani wa kata hiyo |
|
Hili ndiyo kaburi na jeneza kabla maziko na polisi walifika eneo hilo na kuwatawanya wanachi katika eneo hilo la ofisi ya mtendaji |
|
Polisi baada ya kufika katika eneo hilo la ofisi ya mtendaji wa kata ya mhongholo |
|
Gari la polisi katika eneo la msimba |
KATIKA hali isiyotarajiwa na katika kuashiria kukomaa na kukithiri kwa migogoro ya ardhi wilayani Kahama, mkoa wa Shinyanga, wananchi wa mtaa wa Mhongolo, kata ya Mhongolo, wilayani hapa walitishia kuigeuza ofisi ya afisa mtendaji wa kata hiyo kuwa eneo la maziko.
Wananchi hao wakiwa wamejawa na jazba walifika ofisi za mtendaji wa Kata hiyo majira ya saa 7:00 mchana huku wakiwa wamebeba jeneza lililodaiwa kuwa na mwili wa kitoto kichanga cha umri wa mwezi mmoja kilichotambuliwa kwa jina la Rosemary Kanamba na kulazimisha kuchimba kaburi mbele ya mlango wa ofisi ya mtendaji wa kata hiyo aliyetambuliwa kwa jina la Maziku Mbusili.
Wananchi hao walidai kuchukua uamuzi huo kutokana na kile walichodai kuuzwa kwa eneo la makaburi walilotumia kuzika wafu wao miaka ya nyuma huku wakimnyoshea kidole diwani wa kata hiyo Michael Mizubo wakimtuhumu kuhusika kuliuza eneo hilo kinyume cha taratibu na bila idhini ya wakazi wa mtaa wao.
Mmoja wa wananchi wa Kata hiyo Jackson Mselemu akizungumza na wandishi wa habari waliofika katika tukio hilo alisema kuwa walichukua hatua hiyo baada ya kuzuiliwa kuzika nyumbani kwa baba wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Justine Kanamba ambapo uongozi wa Kata hiyo ulidai sheria haziruhusu kwa kuwa kata hiyo imo ndani ya Halmashauri ya Mji wa Kahama.
“Tumeheshimu mamlaka tumetafuta eneo la kuzika tumekosa lakini Mhongolo hapa tumekuwa na eneo lililokuwa mashamba ya Bega kwa Bega tangu miaka ya sabini na diwani wa Kata yetu analifahamu kwani ameongoza miaka kumi na sasa anaendelea kuongoza lakini yeye ndiyo anayefanya vikao vya siri vya kuendelea kuuza maeneo hayo tunamuomba mkuu wa wilaya Fadhil Nkurlu aingilie kati suala hili,” alisema Mselemu huku akiangua kilio.
No comments: