Magogo akionyesha Meneja wa mazao ya misitu Bruno Bahane
KAHAMA WAKALA wa huduma za misitu (TFS) Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
kwa kushirikiana na Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kahama
wamefanikiwa kakamata jumla ya mbao 2904 zilizokuwa zimevunwa na Wafanyabiasha
wa zao hilo bila ya kuwa vibali husika na kuzihifandi katika maghala yao
kinyume cha sheria.
Akiongea na Waandishi wa Habari
ofisini kwake juzi Meneja wa Huduma
za Mazao ua Misitu Wilayani hapa Bruno Bahane alisema kuwa Wafanyabiashara hao
walikamatwa mwezi uliopita katika operesheni iliyojumuisha ofisi yake kwa
kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kahama.
Bahane alisema kuwa kazi ya Wakala wa
huduma za misitu ni kuhakikisha kuwa wananchi wanatunza rasilimali ya
misitu ya Serikali kuu
ikiwa sambamba na kupanda miti kadri inavyohitajika katika jamii ili kutunza
rasimilimali hiyo ya nchi isiwezekupotea kirahisi.
“Mimi kama Meneja wa huduma za Misitu
tulifanya opereheni katika misitu iliyopo katika Wilaya ya Kahama pamoja na
maghala ya wafanyabiashara wa mbao katika miji wa kahama kwa kipindi cha mwezi
mei na kufanikiwa kukamata kiasi cha mbao 2904, Gunia 53 za Mkaa, pamoja na
Magogo 74 na zoezi hili lilifanyika kwa mwezi mmoja”alisema.
Alisema kuwa ili kukabilina na watu
walikuwa wakifanya Biashara hiyo bila ya kuwa vibali maalumu, walilazimika
kushirikaiana na Kamati hiyo ya ulinzi na usalama katika kuvunja maghala ambayo
yalikuwa yakihifadhiwa mizigo hiyo ya magogo ambayo yalikuwa hayana mihuri
kutoka katika ofisi yake.
“Ndugu waandishi wa Habari mbao au
magogo ambayo ni halali kwa mtu kuyamiliki yanatakiwa kuwa na mihuri kutoka
katika ofisi yangu pamoja na nyaraka nyingine za kuambatisha lakini wafanya
biashara hao walikutwa wakiwa na mapungufu kwa asilimia 100na hivyo kupelekea
kutafisha mizigo yao
hiyo”alisema.
Hata hivyo Meneja huyo alisema kuwa
mazao ya misitu sio biashara ambayo niharamu na kuwataka watu wafuate taratibu
za kufanya bisahara hiyo na serikali haitachukua hatua yeyote kwa yule ambaye
atakuwa hayupo kinyume na matakwa ya sheria ya mazao ya misitu.
Aidha Bahane alisema kuwa hali ya
misitu kwa sasa sio nzuri kwani kumekuwa nauvamizi kwa watu kuingia na kufanya
shughuli za kibinadamu kama kuendesha shughuli za kilimo, uchomwaji wa mkaa
pamoja na ufugaji wa mifugo na kuwataka wananchi watoe ushirikinao na ofsi yake
kwa ajili ya kuwabaini watu hao.
Hata hivyo Meneja huyo alisema kuwa
misitu iliyoharibiwa kwa kiwango kikubwa ni ile ya kigosi Moyowosi,
Mkweni, na nyingine ikiwa
katika Halmashauri ya ushetu pamoja na tabora ambayo shughuli za uchomwaji wa
Mkaa, uchanwaji wa Mbao pamoja
na shughuli za kilimo zimekuwa zikifanyika kwa kiwango kikubwa.
|
No comments: