|
Meneja wa shirika hilo Mkoa Maalumu wa
kahama King Fokanya |
|
meneja wa tanesco kahama king akionyesha wanya wa umeme ambazo umbwa na watumishi wake wenye m50 |
|
Moja ya wanya ambazo zinaimbwa na watumishi wa Tanesco kahama wakishirikiana na walinzi |
|
Wanya za umeme |
|
Moja ya kifaa cha kupokea moto ambacho ni moja ya vifaa kilichohalibika |
|
Meneja wa shirika hilo Mkoa Maalumu wa
kahama King Fokanya akionyesha waandishi wa habari wanya ambazo zinazoimbiwa kila mara |
|
Vifaa vya kupokea umeme zikiwa nje ya eneo la ofisi kuu ya tanesco mkoa maalum wa Tanesco |
|
Hizi ni baadhi ya nguzo zaidi ya mia tatu ambazo wakazi wa mji wa kahama bado mahitaji yao ni makubwa zimekwisha sambazwa kwa wateja |
|
Wanya Dil huu kahama |
KAHAMA
UKOSEFU wa vifaa vya kuunganishia
umeme wateja ikiwemo nyaya pamoja na nguzo kwa wateja wa shirika la
umeme(TANESCO) Mkoa maalum wa Kahama unasababishwa na wizi wa vifaa hivyo
unaofanywa na watumishi waliopo katika ofisi ya shirika hilo iliyopo mjin hapa
.
Meneja wa shirika hilo Mkoa
Maalumu wa kahama King Fokanya ameyasema hayo jana wakati akizungumza na
wandishi wa habari ofisini kwake nakuongeza kuwa hali hiyo inapelekea shirika
kushindwa kuwaunganishia umeme wateja wake kwa wakati.
Amesema kuwa shirika hilo
linakabiliwa na changamoto ya uhaba wa nyaya za kuunganisha nguzo hadi nguzo za
mita 50 nakuongeza kuwa shirika likiwa linakabiliwa na changamoto hiyo
watumishi wengine wamekuwa wakitumia mwanya huo wa kuiba vifaa hivyo pindi
vinapopatikana hata kama vifaa hivyo ni vichache.
Ameendelea kusema kuwa lengo kuu la
shirika la umeme(Tanesco) ni kutoa huduma ya nishati ya umeme kwa wateja
wake,lakini mjini kahama lengo hilo limekuwa kinyume na badala yake watumishi
wachache wa shirika hilo wamekuwa wakienda kinyume na malengo ya shirika kwa
kuuza vifaa vya umeme.
Aidha amesema kuwa idadi ya wateja wa
umeme wanazidi kuongezeka siku hadi siku hali hiyo ni kutoakana na mji wa
kahama kukua kwa haraka na kuongeza kuwa matumizi ya vifaa vya umeme yanakuwa
makubwa na kila wakiomba vifaa kwa idadi ya watu hujikuta vikupungua kutokana
na wingi wa wateja.
Hata hivyo amesema kuwa tanesco
kahama mahitaji yake ya nguzo ni zaidi ya 292 huku mahitaji yakizidi kuongezeka
siku hadi siku nakuongeza kuwa jumla ya wateja waliunganishiwa huduma ya
service line ya umeme wako 316.
No comments: