Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango akisoma hotuba kwa niaba ya Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mwakilishi wa Ubalozi wa China nchini Tanzania anayeshughulikia wa Masuala ya Uchumi na Biashara, Lin Zhiyong akizungumza kwa niaba ya balozi wa China wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda akiwasilisha mada inayohusu namna watanzania wanavyoweza kunufaika na fursa za kibiashara na uwekezaji China wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki kutoka China na Tanzania waliohudhuria mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti ya Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo China (CIDRN), Prof. Dr. Li Xiaoyun akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Balozi wa Tanzania nchini China, Mh. Mbelwa Kairuki akizungumzia namna ambavyo watanzania wanaweza wakafaidika na fursa za biashara na uwekezaji nchini China wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akiwasilisha mada inayohusu mahusiano ya kibiashara ya uwekezaji kati ya Tanzania na China kwa mtazamo wa Serikali za Mitaa wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida, Balozi wa Tanzania nchini China, Mh. Mbelwa Kairuki, Waziri Mkuu mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim, Mwenyekiti wa bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo, Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni za Infotech Investment, Ali Mfuruki wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilisha wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mkutano ukiendelea.Balozi wa Tanzania nchini China, Mh. Mbelwa Kairuki pamoja na Waziri Mkuu mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim wakifuatilia mada mbalimbali zilizokua zikiwasilishwa katika mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Profesa Humphrey Moshi kutoka idara ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwasilisha mada inayohusu uhusiano wa China na Tanzania katika masuala ya uwekezaji na biashara wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Maalum ya Uwekezaji (EPZA), Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia akichangia maoni wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mwanachama wa Chama cha Wanafunzi walisomea China (CAAT), Linas Kahisha akielezea uzoefu wake katika fursa za kibiashara nchini humo katika mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Pichani juu na chini ni washiriki kutoka Tanzania na Chini waliohudhuria mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam Mgeni rasmi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi watafiiti kutoka nchini China. Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa ESRF, Prof. Fortunata Makene (kushoto) katika picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Bi. Margareth Nzuki (kulia) mara baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (katikati), Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Bi. Margareth Nzuki na Mwenyekiti ya Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo China (CIDRN), Prof. Dr. Li Xiaoyun katika picha ya kumbukumbu. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (katikati) katika picha ya pamoja na washiriki kutoka TPSF na ESRF na Mshereshaji wa mkutano huo Eng. George Mulamula (kushoto). Baadhi ya washiriki kutoka China wakichukua baadhi ya makabrasha yenye taarifa mbalimbali zilizoandaliwa na ESRF wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida alipowasili katika ufunguzi wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango (katikati) akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kushoto) na Mwenyekiti wa bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo baada ya kuwasili katika mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China.
Mgeni rasmi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango katika picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida mara baada ya kufungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango ametaka kuwapo na uratibu wenye maslahi mapana katika biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China.
Alisema hayo wakati akifungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China. Alisema mahusiano yaliyopo kati ya Tanzania na China ambayo ni ya kihistoria yasitumike vibaya bali yanahitaji kuratibiwa kiuangalifu kwa maslahi ya pande zote mbili.
Aliwataka washiriki wa mkutano huo wa mwaka kujadili kwa makini namna ya kuratibu vizuri vitega uchumi na biashara kwa manufaa ya nchi zote mbili.
Alielezea kufurahishwa kuwapo na mada mbalimbali zinaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China na kusema mada hizo zitumike vyema kuweka misingi mizuri yenye manufaa kwa pande zote mbili.
Aidha aliipongeza ESRF kwa kuona haja ya kuwapo kwa mazungumzo ya aina hiyo na kusema kupitia tafiti mbalimbali taifa hili litaenda mbele katika kujenga uchumi wa viwanda.
Mkutano huo unaohusisha washiriki mbalimbali wa ngazi za juu wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China umeitwa kama sehemu ya mchango wa ESRF katika ujenzi wa uchumi wa viwanda wa Tanzania. “Sisi serikalini tunaridhishwa na juhudi zinazofanywa na taasisi za kitafiti kama hii zenye lengo la kusaidia juhudi za serikali za kuhudumia watu wake na kuongeza ustawi” alisema Mpango.
Mkutano huo ambao unazungumzia mahusiano ya kibiashara na uwekezaji umeelezwa na Mh. Dk Mpango kuwa moja ya mikutano inayotoa fursa za kuangalia uwekezaji wenye tija unaozingatia maslahi mapana ya mataifa husika.
Alisema Tanzania na China zina uhusiano mzuri wa kihistoria na hadi sasa na kwamba kinachostahili ni kuoanisha uhusiano huo na kuuweka katika hali bora zaidi za kunufaisha pande zote mbili.
Baadhi ya miradi mikubwa ambayo Tanzania imesaidiwa na China ni pamoja na ujenzi wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) na kiwanda cha Urafiki; kuanzishwa kwa shamba la mpunga la Mbarali; kiwanda cha sukari cha Mahonda na mgodi wa mawe wa Kiwira.
Kwa sasa China ni moja ya taifa lililo na uwekezaji mkubwa nchini Tanzania pia ikifanya shughuli nyingi za ujenzi zenye gharama kubwa kama daraja la Kigamboni na barabara.
Naye Mwenyekiti wa bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo, akimkaribisha Mheshimiwa Waziri Mpango alisema kwamba alisema kwamba mkutano huo umeandaliwa kwa pamoja kati ya ESRF na Chuo kikuu cha Kilimo cha China.
Alisema mkutano huo umewaleta pamoja wanazuoni wa Kichina na Kitanzania kuangalia mahusiano yaliyopo na kutengeneza mustakabli bora wa namna ya kushirikiana.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida amesema kwamba mkutano huo ni sehemu ya juhudi za kusaidia serikali kwa njia ya utafiti ambapo majibu yanatumiwa kutengeneza sera au majibu ya changamoto mbalimbali. Mkutano huo ulifungwa na Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Dkt. Salim Ahmed Salim.
No comments: